Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

YATOE MAISHA KAMA HUTAKI KUYAPOTEZA!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumapili, Septemba 3, 2023 
Juma la 22 la Mwaka
___________________

Yer 20:7-9; 
Zab 62:2-6, 8-9; 
Rum 12;1-2; 
Mt 16:21-27
___________________

YATOE MAISHA KAMA HUTAKI KUYAPOTEZA!

“Mbegu ya ngano isipo anguka katika ardhi na kufa, inabaki kuwa hivyo hivyo, lakini ikifa, inazaa matunda zaidi” (Yn 12:24). Mungu alimwahidia Abrahamu mafanikio na kuwa na watoto kama nyota za Mbinguni, alimwambia pia amtoe sadaka mwanae wa pekee Isaka, ambaye ndiye aliyekuwa afanye ahadi yake itimie. Jaribio kama hili linaweza kukabiliwa na mtu mwenye kuamini kama Abraham. Leo Yesu ana ahidi kuwatambulisha wafuasi katika maisha “atakaye nifuata mimi atakuwa na nuru ya uzima…hataona kifo…hatakufa.” (Yn 8:12, 51-52)

“Mungu ni mwema kwa walio na haki, kwa watu walio na mioyo safi” (Zab 73:1). “Mwamini yeye na mruhusu yeye afanye kazi atakuwa sababu ya wewe kungaa kama jua”. (Zab 37:5-6). Mungu alimwita Yeremia “Nenda utume wowote nitakao kupa, na utasema chochote kile nitakacho kuamuru useme,” wakati alivyo kuwa na woga, akilalamika kwamba yeye ni mdogo na kwamba hafahamu kuongea, Bwana alimhakikishia: “usiogope..nitakuwa nawe kukulinda…watapigana nawe lakini hawatakushinda kwani nitakuwa nawe kukuokoa” (Yer 1:7-8, 19). Yeremia alikubali, watu hawakumuelewa, aliambiwa akae kimya na hata alipigwa na kufungwa gerezani. Katika hali hii Yeremia akapaza kilio chake kwa Mungu, ambapo kinasikika katika somo la kwanza “Yahweh, uliniita mimi nami nikaitika”. Nabii anafananisha wito wake kama vile mvulani anavyo mchumbia mwanamke kwa maneno mazuri, na baada ya kukubali maneno yake, na kutimiza haja ya moyo wake, anaachwa. Hivyo anajikuta akilaani kwanini alianguka kwenye upendo wa uongo. Katika hali hiyo ya taabu, Yeremia anajazwa na hasira kwa mpendwa wake na anasema “sintamfikiria tena Mungu na wala sintaongea tena juu ya jina la Mungu”. Lakini kwasababu alisha uonja upendo wa Mungu, Yeremia anashindwa kujinasua yeye ambaye alishaitika wito wake. Ndani ya moyo wake kuna waka moto ambao hawezi kuuzima. Pamoja na mateso anayopata na wakati mgumu alionayo hawezi kuacha utume wake.

Katika somo la pili Paulo anawaasa wakristo wasije wakashikamana na mtazamo wa “ulimwengu huu”, namna ya kuwaza na jinsi dunia inavyo dhani ni hekima kwa wote. Mkristo hapaswi kuwaza na kujiingiza kwenye maadili ambayo dunia inadhani ni sawa tu kwa wote. Mkristo anapaswa kutambua, kuwa mtulivu, na kuwa na akili ya upya muda wote, tabia ambayo inakubalika kwa Mungu hata kama watu hawaitaki au haionekani yenye maana kwa watu.

Katika somo la Injii Yesu ameamua kurarua matarajio ya wafuasi. Mawazo ya mitume yalikuwa ni kupata sehemu nzuri ya heshima kwasababu ya mawazo yaliyo kuwa yameshasemwa na vongozi wa Wayahudi, kuwa na Amani na ulimwengu mpya wenye haki. Waliamini kwamba mwisho wa ulimwengu ulikuwa karibu na mkuu wao alikuwa ni Kristo, Masiha anaye subiriwa “Mwana wa Daudi”. Tangu kungara sura, na kumpa Petro funguo, walimfuata Yesu ili waweze kushuhudia uhalisia wa ndoto zao za utukufu. 

Yesu akijua hali hii ya mtazamo mbaya kuhusu yeye, anaamua kubadilisha mitizamo yao. Anasema kwa wazi kwamba yeye hatembei kuuendea utukufu huo, bali kwenda Yerusalemu kuteswa, kuuwawa na siku ya tatu atafufuka. Mitume hawakuweza kulielewa hili., kwasababu walikuwa wameshajifunza kutoka kwa Marabi kwamba Masiha hawezi kufa, na kwamba waliowema watafufuka na kuingia katika utawala wa huyu Masiha atakaye kuja, na hivyo Petro anamjibu. Petro hataki kusimama katika barabara inayo ongoza katika kutofanikiwa. Anajaribu kumbadilisha Yesu abadilishe mtazamo wake.

Jibu la Yesu “rudi nyuma yangu shetani”. Petro hakuwa anatenda kosa dogo. Alikuwa anafuata njia inayo pingana na Bwana. Alikuwa akitenda kama zile tabia za shetani aliye jaribu kumshawishi Yesu aelekeze mawazo yake katika ufalme wa kidunia, na kuwa na mamlaka ya kuangamiza. Alimuongoza katika mlima mkubwa nakumuonesha falme zote kwa mara moja na utukufu wa ulimwengu na kumwambia “yote haya nitakupa, kama utapiga goti na kunisujudia mimi” lakini Yesu akajibu “nenda zako shetani” (Mt 4:8-10). Sasa kishawishi hiki hiki –katika hali ya juu pia na Petro-hawezi kuacha bali kujibu kwa ukali ule ule.

Katika Injili ya jumapili iliyopita, Simoni Petro alikuwa ameitwa na Yesu kwamba yeye ni jiwe linaloishi la kanisa lake kwasababu alikuwa amepokea ufunuo wa Baba yake, alipokea Imani na mpango wake na amekiri Imani juu ya Mwana wa Mungu aliye hai. Sasa anajikuta yeye mwenyewe akianguka kwani aliruhusu akili ya kibinadamu imtawale. Baada ya kumkemea Petro anawageukia pia na wengine na kuwaeleza wazi.

Mambo matatu muhimu katika kubadilika “Jikane mwenyewe uchukue msalaba wako unifuate”. Kwanza, kujikana mwenyewe maana yake kila mfuasi aache kujifikiria mwenyewe kwanza. Neno hili ni ni muhimu sana katika ulimwenu wetu wa ubinafsi na umimi. Hali ya kujali mambo binafsi zaidi yanazingatiwa hata katika jambo dogo la upendo kwa wengine. Mfuasi yeyote wa Kristo anaitwa kwanza kabisa kuacha mambo yeyote ya ubinafsi, hata kujipendelea mwenyewe kiroho bila kuwaombea wengine. Daima anapaswa kutenda mapenzi ya Mungu. 

Pili, “kuchukua msalaba” haina maana ya kuvumilia mateso kidogo au makubwa ya maisha kama sehemu ya kumfurahisha Mungu. Mkristo hatafuti mateso bali upendo. Msalaba ni ishara ya upendo na zawadi kuu. Kuubeba na kumfuata Kristo maana yake umeamua kufuata ile njia yake ya upendo kwa ajili ya wanadamu. Kutoa maisha kwa ajili ya wengine, kufariji, hata kifo na mateso kwa ajili ya kubaki katika kuishika injili yake. 

Na hatimaye, “Nifuate mimi” maana yake kushiriki’ kuchagua kumfuata, kwa mapendo na kukabidhi maisha yote kwa Mungu. Kutoa maisha yako kwa mapendo na kuwa naye.

Yesu anamalizia na sababu tatu za kuwasihi wafuasi wake wapokee hayo maelekezo: kwanza, anaye toa maisha yake kwa ajili ya mwingine hayapotezi bali anayapokea. Ni yule tuu mwenye ujasiri wa kupoteza mbegu ya uzima wa maisha yake, kutupwa ardhini, “kuilinda” “ataipokea”. Pili, maisha ya ulimwengu huu yanaisha mara moja. Ni ya kupita, ni hafifu, na sio vizuri kuyategemea kama vile ni ya milele. Tatu, ni zawadi ya mwisho, Mungu hataangalia majina au mangapi tumejitengenezea mbele za watu au kwa jina letu, bali ni kazi ngapi za mapendo zinazo toka katika majina yetu. Kwa njia hiyo utakatifu wetu haupimwi na sifa wanazo sema watu juu yetu bali kazi njema za mapendo na muonekano wetu mbele ya Mungu.

Sala: Bwana, nakupenda wewe. Ninakuomba nisiogope kujikana mwenyewe, kuchukua msalaba wangu, nakukufuata wewe. Ninakuomba nikuwe katika upendo na wewe, ili niweze kuishi maisha yangu kwa upendo wako. Ninakuomba matendo ya maisha yangu yalindwe na uhusiano wangu na wewe. Ninakuomba nifuate sadaka yako ya kujitoa bila kujibakiza, na kuwa sadaka kwa watu wote. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment