MASOMO YA MISA, JUMATANO, SEPTEMBA 17, 2025
JUMA LA 24 LA MWAKA
________
________
SOMO I
1 Tim 3: 14-16
Nakuandikia hayo, nikitaraji kuja kwako hivi karibu. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu:
Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulika kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa,
Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.
Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 111: 1-6
(K.) Matendo ya Bwana ni makuu. Au: Aleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Matendo ya Bwana ni makuu.
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. (K.)
Kazi yake ni heshima na adhama,
Na haki yake yakaa milele.
Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
Bwana ni mwenye fadhili na rehema. (K.)
Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,
Kwa kuwapa urithi wa mataifa. (K.)
________
Lk 6: 63,68
Aleluya, aleluya,
Maneno yako, Bwana, ni roho na uzima.
Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.
________
INJILI
Lk. 7:31-35
Wakati ule: Jesu aliwaambia makutano, "Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki, nao wamefanana na nini? Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, 'Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.'
Kwa kuwa Johane Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, 'Ana pepo.' Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mwasema, 'Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.' Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote."
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
________
Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment