“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Septemba 29, 2023
Juma la 25 la Mwaka Wa Kanisa
Sikukuu ya Malaika Wakuu Gabriel, Mikaeli na Rafaeli
Dan 7: 9-10, 13-14 au Uf 12: 7-12;
Zab 137: 1-5;
Yn 1: 47-51
MALAIKA KATIKA MAISHA YETU!
Leo tuna adhimisha sikukuu ya Malaika wakuu watatu ambao majina yao
yanatajwa katika maandiko: Mikaeli, Gabriel na Rafaeli. Hawa malaika wanaitwa
“Malaika Wakuu” maana yake ni wakuu kwasababu wana utume maalumu waliopewa na
Mungu. Sikukuu hii ya malaika inatukumbusha kwamba vitu vinavyo onekana na
kushikika ni sehemu ndogo sana ya ukweli halisi na hatuwezi kujifanya kujua
kila kitu. Siku hizi tunaweza tusitembelewe na malaika kama alivyomtembelea
Bikira Maria wakati wakutangazwa kuzaliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo au
kipindi cha kutangaza ufufuko wa Yesu, au kipindi cha Tobiti, lakini Mungu
anaendelea kuwasiliana nasi kwa namna ya pekee. Swali ni kwamba, mimi nipo wazi
kiasi ghani Mungu anapotaka kuongea nami? Hasa kwa njia ya neno lake? Je
unaamini uwepo wa malaika hawa, je unaomba wakuombee? Mungu anataka kuwatumia,
tafuta msaada wao katika maisha yako.
Leo sala yetu iwe, Baba wa Mbinguni, umetupa malaika wakuu ili kutusaidia
sisi wahujaji hapa duniani. Mtakatifu Malaika Mikaeli ni kinga yetu, namuomba aje
kunisaidia, awapiganie wapendwa wangu wote, na atukinge na hatari. Mtakatifu
Malaika Gabrieli ni mjumbe wa habari njema, namuomba anisaidie kusikia sauti
yako na anifundishe ukweli. Mtakatifu Malaika Rafaeli ni malaika anaye ponya,
ninamuomba anipe uponyaji wa yale yote ninayohitaji kuponywa na ya kila mmoja
ninaye mfahamu, nyanyua juu katika kiti chako cha neema na utupe tena zawadi
yako ya kupona na kuwa huru. Tusaidie Bwana tuweze kutambua kwa ukamilifu
kabisa, ukweli wa Malaika Wakuu na hamu yao yakutaka kututumikia.
Sala: Bwana, tunakushukuru kwa zawadi ya malaika watakatifu tunao wakumbuka leo. Tunakushukuru kwa msaada
wao wa nguvu katika maisha yetu. Malaika Watakatifu tuombee sisi, tufundishe na
kutulinda. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment