“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Septemba 19, 2025
Juma la 24 la Mwaka
1 Tim 6: 2-12;
Zab 48: 6-10, 17-20;
Lk 8: 1-3
KUWA NA YESU!
Luka anatuambia kuhusu kazi kubwa waliyo ifanya idadi kubwa ya wanawake
katika kutegemeza utume wa Bwana wetu na Wafuasi. Pamoja na tofauti zao kati ya
wanawake, lakini inaonekana wote walikuwa na kitu cha pamoja kwamba: Yesu
amewaponya kimiujiza kwasababu ambayo hakuna jibu sahihi kutoka kwa Mwanadamu.
Katika hali ya kufikirika, kundi lililo fuatana na Yesu lilitoa ushahidi na
kumtambulisha Yesu kama Kristo Masiha. Wanawake hawa hawakuwa watu
wasiojitambua waliofuata tu, walikuwa watu waliokuwa hai katika kutangaza
Injili ya Ufalme wa Mungu. Wakati Yesu alivyo watuma wale kumi na wawili (Lk 9:
1-6) na wale sabini na mbili (Lk 10: 1-12). Aliwaambia wasichukue chochote. Hii
ni kwasababu walikuwa wafanye utume kwa wale waliowafuata, ambao kati yao
waliishi miongoni mwao. Tunapaswa tuwe tunafanya walichofanya wanawake hawa.
Walimpenda Yesu sana, walimtumikia yeye na wafuasi wake kwa vile walivyokuwa
navyo.
Je unadhani Yesu alihitaji msaada wao? Hapana. je, alihitaji chakula chao?
Hapana. Kama Yesu angependa angeweza kuchukua tu kipande cha mkate katika
mkoba, na pale watakapo hisi njaa yeye na wafuasi wake Yesu angeiongeza hata
kuwa kikapu kilicho jaa. Kwanini hakufanya hivyo? Hii ni kwasababu kama kuna
kitu anachopenda Yesu zaidi kuliko kuwalisha watu, ni wakati watu wanampa yeye
kwasababu wanampenda. Haitaji yote hayo, bali anapenda kupokea. Inampa furaha
kubwa tukimpenda. Yesu hajapungukiwa chochote, tukimpenda na kumtumikia ni
faida kwetu sisi kwamba tunampendeza Bwana, nasi tunajipatia Baraka kwa ajili
ya roho zetu. Tunajua kwamba sala zetu hazi muongezei Mungu kitu, ila za faa
kwa ajili ya wokovu wetu. Tumtumikie Mungu kwa uchaji katika wema na kweli ili
tujipatie utakatifu wa roho zetu.
Sala: Bwana, ninaomba uje unisamehe mimi, niponye mimi nikurudie wewe kwa
shukrani kuu, nikufuate wewe popote pale uniongozapo. Yesu nakuamini wewe.
Amina

No comments:
Post a Comment