"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Julai 15, 2023
Juma la 14 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mtakatifu Bonaventure, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
Mwa 49: 29-33, 50:15-25;
Zab 105: 1-4, 6-7 (R) Ps. 69:32;
Mt 10: 24-33.
MSIOGOPE
Tunaishi katika dunia yenye hatia ambamo visa na matukio tusioyatarajia yanatukumba. Tumejawa na hofu ya nini kitatutokea baadae, tupatapo ajali, tunapofilisika kiuchumi, au kama kuna vita na mvutano n.k. Tukiwa tumejawa na mawazo haya mbele yetu, tunajikuta tukiyaweka maisha yetu katika bawaba za hofu na woga, na pia kuyadidimiza matumaini yetu kwa Yesu.
Katika kukabiliana na hili Yesu anatutia nguvu akituambia “msiogope”, na anatupa ujasiri tunaouhitaji katika kujinasua na bawaba za hofu na woga, na pia anayaweka matumaini yetu katika mapenzi yake matakatifu. Mungu pekee anatosha kukidhi kiu yetu ya kiroho, akituwashia daima mwanga wa matumaini kumpenda na kumtumaini yeye peke yake.
Hivyo, kwa matumaini hayo, yaliyojengwa imara katika Mungu pekee, tunapokea fadhila ya ujasiri, ambayo inatuwezesha kupambana na changamoto zote za dunia na kutangaza neno la Mungu duniani bila hofu. Fadhila hii ya matumaini itawalayo ndani mwetu, itatufanya kuwa kama Kristo mwenyewe na kwa moyo wenye furaha tutamuitikia yeye tukisema: “mimi hapa, nitume mimi” “Hivyo basi tunaalikwa kujitahidi kumkiri Kristo duniani bila kijibakiza na bila hofu na pia tuombe ili tuweze kustaili alichotuandalia huko mbiguni.
Sala: Ee Bwana uondoe dhambi yangu na hatia yangu; fukuza hofu ndani ya roho yangu, na uijaze pendo lako, ili nipate kuwa mfuasi wako mwema. Amina.

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment