Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, JULAI 2, 2023


MASOMO YA MISA, JUMAPILI, JULAI 2, 2023
DOMINIKA LA 13 LA MWAKA


MWANZO:
Zab. 47:2
Enyi watu wote, pigeni makofi, mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe.


SOMO 1 
2 Fal 4:8-11,14-16

Ilikuwa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; nave akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu w’a Mungu. Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa na itakuwa, atujiapo, ataingia humo. Ikawa siku moja akafikia huko, akaingia katika chumba kile akalala. Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee. Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI 
Zab. 89 : 1-2, 15-18 (K) 1

(K) Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. (K)

Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,
Ee Bwana, kuenenda katika nuru ya uso wako.
Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,
Na kwa haki yako hutukuzwa. (K)

Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,
Na kwa radhi yako pern be yetu itatukuka.
Maana ngao yetu ina Bwana,
Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli. (K)


SOMO 
Rum. 6:3-4,8-11

Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika

wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


SHANGILIO 
Mt. 11:25

Aleluya, aleluya, 
Nakushukuru, Baba, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. 
Aleluya.


INJILI 
Mt. 10:37-42

Yesu aliwafundisha mitume wake hivi: Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeave nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia. haitampotea kamwe thawabu yake.

Neno la Bwana........Sifa kwako Ee Kristo


Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment