Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUSIMAMA IMARA KATIKATI YAVIPINGAMIZI!


"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Julai 11, 2023
Juma la 14 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Benedikto, Abati

Mwa 32:23-33; 
Zab 16:1-3, 6-8; 
Mt 9:32-37


KUSIMAMA IMARA KATIKATI YAVIPINGAMIZI!

tukijaribu kufikiria kuhusu mpangilio na muunganiko ulivyo katika Kanisa Katoliki, tukijaribu kurudi tangu mwanzo wa kipindi cha mitume, mafundisho yake, msimamo wake, tamaduni zake zinazoleta faraja, Sakrament mbali mbali, umoja wa mafundisho yake, uongozi wa asili ya mitume, mpangilio wake katika kazi ya watakatifu na mashahidi, liki neemeshwa na naombezi ya Mama wa Bwana wetu Yesu Kristo, tukitizama pia umoja wa uwepo wa mkombozi wetu juu ya Altare, tunajisikia Kanisa hili, Moja, Takatifu, Katoliki la Mitume limetupatia mpangilo mzuri sana na kuwa jua linalo angaza kuondoa giza.

Ni hakika, tangu mwanzoni kabisa Kanisa limepingana kwa hali zote na mafundisho ya uongo yaliojaribu kuharibu ujumbe halisi wa mapokeo ya Mitume. Kanisa limebaki aminifu na litaendelea kubaki aminifu kwa kiini cha mafundisho ya Imani juu ya Kristo.
Sisi pia mara nyingi tumekutana na watu wengi wanaotuuliza maswali kuhusu Imani yetu, na zaidi sana kuhusu kumheshimu Bikira Maria na kumuomba atuombee na pia kuhusu watakatifu au kuhusu Sakramenti na zaidi sana Sakramenti ya Kitubio na mengine mengi. Huwa tunakabiliano nao vipi? Leo Injili inatufundisha jinsi ya kukabiliana na hali hizo katika maisha yetu.

Injili inatuambia kwamba, mara nyingi Yesu aliwaonea huruma wale wasiokuwa na msaada, walioteseka na wale waliotengwa. Watu mashuhuri hawakupenda Yesu awape nafasi ya kwanza wadhambi na kula pamoja nao. Lakini Yesu hakuwasikiliza walivyo mlaumu. Kama Yesu tunapaswa kuwa imara tunapotaka kuyumbishwa juu ya Imani yetu na tunu za Injili. Kanisa Katoliki sio Kanisa la Biblia tu, lina Mapokeo Matakatifu (mafundisho ya mitume na mababa wa Kanisa, Mafundisho ya Mababa watakatifu n.k), bahati mbaya au kwakutotaka kuyafahamu wengi wanao uliza maswali haya, hawayajui na zaidi sana hawapo tayari kujifunza kwasababu kwao kama kitu hakijaandikwa kwenye Biblia sio kitu kizuri. Kanisa Katoliki chanzo cha mafundisho yake yamejikita katika Maandiko Matakatifu na Mapokeo Matakatifu (Sacred Traditions), kwahiyo Kanisa Katoliki sio dini ya Biblia tu. Tunapaswa kuwa Makini kuhusu Imani yetu, tusiyumbishwe , tushikilie imara kile tunacho amini, mafundisho yalio asili ya Imani yetu.

Tafakari leo, jinsi tunavyofikiri kuhusu wengine. Je, upo kama ule umati walioona Yesu akifanya miujiza na kushangazwa kwa uzuri wa yale aliokuwa akifanya? Au upo kama Mafarisayo ambao walipenda kupindisha ukweli na kutoa majibu yasio kweli? Jiunge na imani kama hawa watu wa kundi ili uweze kuwa na furaha ndani ya Kristo.

Sala: Bwana, ninatamani kuwa na moyo wa unyenyekevu na Imani sahihi. Nisaidie niweze kukuona na kushangazwa na miujiza yako unayofanya katika maisha yangu ya kila siku. Yesu nakuamini wewe. Amina 


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment