Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

IMANI NA UPONYAJI


"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Julai 10, 2023
Juma la 14 la Mwaka

Mwa 28:10-22;
Zab 90:1-4, 14-15;
Mt 9:18-26


IMANI NA UPONYAJI 

Leo katika Injili, tunaona matukio mawili ya miujiza wa kuponya. Hawa ni watu walio muhitaji Yesu ili waponye. Tunakutana na watu wengi wanao ulizia kuhusu upendo wa Mungu na kwanini Mungu hawaponyi? Kuna wengine pia wanajiuliza pia kuhusu Imani yao wenyewe wanajisikia kama wangekuwa na Imani kubwa zaidi kwa Mungu ungekuta Mungu amesha waponya.

Kijana mmoja aliitwa Stefano wa umri wa miaka 18, alipata ajali ya gari na alipata hitilafu katika ubongo wake kiasi cha kushindwa pia kuongea vizuri. Na mwaka mmoja baadaye akadondoka kutoka kwenye paa la nyumba, akapooza kuanzia kwenye kiuno kushuka chini. Daktari akamwambia Stefano hutaweze kutembea tena. Lakini Stefano akamwambia Mungu ameniambia huu ni muda wake wakuniponya. Imani yake ilikuwa ya kweli na hakika, hakuwa na mashaka yeyote kwamba Mungu atamponya. Siku moja watu walikusanyika kumuombea, yeye alienda mbele kwakujivuta na kukaa mbele yao, wakamuombea na kusali sana lakini hali yake ikabaki vile vile. Baada ya hapo watu walimuhuzunikia sana kwa hali yake. Walishangaa sana kwamba alikuwa na Imani na walijiridhisha kwamba atapona lakini wakashnga sasa Imani yake imekuwaje tena? Baada ya mkutano wao wakamkuta Stefano wakashngaa. Alikuwa hayupo vizuri lakini Imani yake ilikuwa haijayumbishwa. Kwa sauti ya huzuni Stefano alisema “haikuwa muda wangu wakupona lakini siku moja nitasimama na kukimbia”.

Hakika tuna muujiza hapa. Muujiza haukuwa katika miguu yake, bali ulikuwa muujiza wa roho yake. Mwanga wa Yesu ulikuwa ukingaa ndani ya roho yake. Na zaidi ya yote, uponyaji wa mwili ni kwaajili ya muda mfupi. Bali uponyaji wa roho na Uponyaji wa Imani unadumu kwaajili ya uzima wa milele. Tumuombe Mungu atusaidie kushughulika zaidi na uponyaji wa Imani yetu na maisha yetu ya kiroho ili tuweze kupata nafasi katika maisha ya milele.

Je, unatambua kina cha nguvu ya Yesu? Je, unatambua upendo wake unamsukuma atumie nguvu yake kwa ajili ya uzuri wako? Kutambua na kukubali ukweli huu utabadilisha maisha yako na kumruhusu yeye afanye miujiza ya Imani.

Sala: Bwana, ninaamini juu ya nguvu zako kamili juu ya vitu vyote na mamlaka yote kuhusu maisha yangu. Nisaidie mimi nikuamini wewe na kuamini juu ya upendo wangu kwako. Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment