Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MAFUMBO YA UFALME WA MUNGU!



"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Julai 27, 2023 
Juma la 16 la Mwaka

Kut 2:1-15; 
Zab 69:3, 14, 30-31, 33-34; 
Yer 2:1-3, 7-8, 12-13
Zab 36:5-10 (K) 9
Mt 13:10-17


MAFUMBO YA UFALME WA MUNGU!


Katika maisha, mara nyingi tunadadisi, vilevile tunashangazwa na fumbo. Pale tunapopoteza hali ya fumbo katika dini ndipo Mungu anakuja kuwa kama wazo tu. Katika nyakati ya Yesu, Mungu amekuwa kama kitu kilichopo akilini mwa watu tu na si mioyoni mwao. Yesu anamnukuu nabii isaya katika injili: “maana mioyo ya watu hawa inakuwa mizito, na kwa masikio yao hawasikii vyema na macho yao wameyafumba.” Aliwaambia wanafunzi wake kwamba si kila mmoja ataelewa mifano. Yesu aliongea hayo kutokana na uzoefu. Alielewa kwamba baadhi yao ambao walisikia mifano yake walikataa kuielewa, si kwamba akilio zao hazikuweza kuelewa, bali, walifunga mioyo yao kwa yale aliyokuwa akisema Yesu. Walikuwa wameweka nia ya kutokuamini.

Mungu huweza kufunua siri za ufalme wake kwa mnyenyekevu na mtu anayemtegemea na kukiri uhitaji wa Mungu na ukweli wake. Mifano ya Yesu itatuangaza sisi kama tukiipokea kwa akili na mioyo radhi na kuwa tayari kukubali itupe changamoto. Neno la Mungu linaweza tu kuota mizizi katika moyo unaokubali na kuamini na kujitoa kwa hiari.

Sala: Bwana nakukaribisha moyoni na akilini mwangu uniangaze, unipe changamoto na unibadilishe. Amina.

Copyright ©2013-2023©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment