“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila Siku
Ijumaa, Juni 16, 2023,
Juma la 10 la Mwaka wa Kanisa
Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Kumb 7: 6-11;
Zab 103: 1-4;
1 Yn 4: 7-16;
Mt 11: 25-30
MOYO UNAO WAKA MAPENDO!
“Huu ni upendo si kwamba sisi tulimpenda Mungu kwanza bali yeye alitupenda
sisi kwanza akamtuma mwanaye ulimwenguni kama sadaka kwaajili ya dhambi zetu”
(1 Yn 4: 10). Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni sherehe ya upendo wa
ukombozi wa Mungu wetu. Mungu anayetupenda alimtoa mwanaye aje ulimwenguni kama
sadaka kwaajili ya ukombozi wa Ulimwengu. Upendo huu unaoneshwa katika moyo wa
mwana wa Mungu. Neno “moyo” linasimama kama upendo wa mtu. Na hivyo watu husema
“Nakupenda kwa moyo wangu wote” na wakati tunapo sheherekea sikukuu ya Moyo
Mtakatifu wa Yesu kanisa linatuhimiza kutafakari juu ya upendo wa Mungu, upendo
uliofunuliwa ndani ya mwili wa Mwanaye Yesu Kristo.
Ni Mungu aliyewachagua wa Israeli kuwa watu wake. Aliwabariki na
akawachagua kuwa watu wake kati ya mataifa mengi. Si kwasababu walikuwa na
nguvu kuliko wengine lakini kwasababu ya upendo wake. Hili ndilo Musa
alilowafundisha watu wa Israeli. Anawakumbusha juu ya upendo wa Mungu juu yao.
Upendo wa Mungu kwa watu wake hauna mwisho na hauna masharti. Aliwapenda watu
wake pamoja na mapungufu yao na makosa yao. Na hata hivyo ubinadamu uliponaswa
na dhambi alimtoa mwanaye wa pekee kwajili yetu. Kwahiyo tunapaswa kuuzoea
nakuupenda upendo huu ili tuweze kuuelewa zaidi na kuwa watu wakweli wanotamani
kuwa na Mungu daima. Ili tuweze kumpenda kwa moyo wetu wote na akili yetu zote.
Kwahiyo katika sikuu hii ya moyo Mtakatifu wa Yesu, tunamshukuru Mungu kwa
upendo wake mkubwa kwetu anaotuonesha kila siku. Tuupende na kuushi upendo huu
ndani mwetu ili tuweze kuwashirikisha na wengine.
SALA: Moyo Mtakatifu wa Yesu, utuhurumie. Ninakushukuru Bwana wangu kwa
kunipa yote hayo. Hakuficha kitu kwangu na unaendelea kunigawia maisha yako kwa
ajili yangu na kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ninaomba nipokee yote unayonipa bila
kubakiza chochote kutoka kwako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment