MASOMO YA MISA, JUNI 04, 2023
SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU
Jumapili baada ya Pentekoste
MWANZO:
Asifiwe Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu;
kwasababu ametufanyizia huruma yake.
SOMO 1
Kut. 34 : 4-6, 8-9
Musa aliinuka na mapema asubuhi, naye akakwea
katika mlima wa Sinai, kama Bwana alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za
mawe mkononi mwake.
Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama
pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake,
akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa
hasira, mwingi wa rehema na kweli; Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa
chake hata nchi, akasujudu. Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana,
nakuomba, Bwana, uende kati yetu maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe
uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Dan. 3:52-56. (K) 52
(K) Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu:
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Limehimidiwa jina lako takatifu, tukufu;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
Umehimidiwa katika hekalu la fahari yako
takatifu;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa juu ya kiti cha ufalme wako;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
Umehimidiwa utazamaye vilindi, uketiye juu ya
makerubi;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa katika anga la mbinguni
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
SOMO 2
2 Kor. 13 :11-14
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfariji-
ke, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja
nanyi. Sali- mianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wawasalimu. Neema ya
Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu. na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi
nyote.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
SHANG1LIO
Ufu. 1 :8
Aleluya, Aleluya,
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu
ambaye yupo, aliyekuwako, na atakayekuja.
Aleluya.
INJILI
Yn. 3:16-18
Yesu alimwambia Nikodemu: Kwa maana jinsi hii
Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana
ulimwenguni ili auhu- kumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu
hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment