Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUMATATU, JUNI 26, 2023


MASOMO YA MISA, JUMATATU, JUNI 26, 2023
JUMA LA 12 LA MWAKA



SOMO 1
Mwa. 12 : 1-9

Bwana alimwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 

Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano aiipotoka Harani. Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia, na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.

Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki; akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pandc za kusini.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.




WIMBO WA KATIKATI
Zab. 33 :12-13,18-20,22 (K) 12

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
watu aliowachagua kuwa urithi wake.


Heri watu aliowachagua kuwa urithi wakc.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia. (K)

Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao faadhili zakc.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)

Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiyc msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe. (K)



SHANGILIO 
Zab.l9:8

Aleluya, aleluya, 
Amri ya Bwana ni sali, 
huyatia macho nuru. 
Aleluya.




INJILI
Mt. 7:1-5

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachoimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lake mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Injili ya Bwana........Sifa kwako Ee Kristo


Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment