Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 27, 2023


MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 27, 2023
JUMA LA 12 LA MWAKA


SOMO 1
Mwa. 13 : 2, 5-18

Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha na kwa dhahabu. Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng’ombe na kondoo, na hema. Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. Je! nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto. 

Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapowenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma. Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.

Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, na uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii, katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. Basi Abramu akajongeza hema yake akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.




WIMBO WA KATIKATI
Zab. 15:1-5 (K) 1

(K) Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?

Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Ni mtu aendaye kwa ukamilifu na kutcnda haki 
asemaye kweli kwa moyo wake. (K)

Asiyesingizia kwa ulimi wake,
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa.
Bali huwaheshimu wamchao Bwana. (K)

Hakutoa fedha yake apatc kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo 
Hataondoshwa milele. (K)



SHANG1LIO 
Zab. 119:105

Aleluya, aleluya, 
Neno lako ni taa ya miguu yangu, 
na mwanga wa njia yangu. 
Aleluya.




INJILI
Mt. 7:6,12-1

Yesu aliwaambia wanafunzi wake; Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeeni vivyo hivya hiyo” maana hiyo ndiyo torati na manabii. Ingieni kwa kupitia mlango uliyo mwembamba, maana, mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. 


Injili ya Bwana........Sifa kwako Ee Kristo


Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment