Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MUNGU ALIYE NA MSIMAMO NA MWENYE HURUMA




ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumapili, Juni 18, 2023
Juma la 11 la Mwaka


Kut. 19:2-6; 
Rum. 5:6-11; 
Mt. 9:36-10:8


MUNGU ALIYE NA MSIMAMO NA MWENYE HURUMA

Kwenye Injili ya Jumapili hii, Yesu alipowaoona umati wa watu aliwaonea huruma. Walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji au kiongozi. Jumapili hii pia twaadhimisha ukumbusho wa mababa wote. Basi nawatakieni mababa wote heri na mafanikio mema kwa siku kuu yao na tunawaombea wote, walio karibu na wale walio mbali, pamoja na kuwakumbuka wale waliotuacha. Kwa njia ya pekee tuwaombee akina baba kwenye parokia zetu. Nitaanza mahubiri haya kwa hadhithi moja. Kwenye familia mmoja kulikuwa na mtoto mvulana aliyekuwa aliyekuwa na tabia ya kutotii amri za kinyumbani. Basi siku moja baba yule akamwita mtoto wake akamwambia: wakati utakayevunja amri tena nitakufungia nje kwenye ghala. Punde si punde, yule mtoto akavunja amri tena. Ndipo babaye akampeleka mtoto ghalani na kumfungia mle. Baada ya kufanya hivyo baba akahuzunika asile au kunywa chochote. Ndipo mama akamwambia, mimi naelewa vile unavyofikiria. Nakusihi usimtoe mtoto kutoka ghanani, kwa sababu ukimtoa ataendelea kutotii amri zako. Hatakuheshimu kamwe. Baba alifikiria kuelewa kwamba mama amesema hakika. Mwishowe yule baba akamwonea mwanae huruma, na badala ya kumfungulia akachukua blanketi na mikate ya chapati na akaenda kule ghalani kulala naye usiku huo.

Masomo ya Jumapili hii hasa yatufumbulia Mungu aliye kama yule baba kwenye hadithi kwa ajili ya msimamo wake na pia huruma wake.Kwenye Somo la Kwanza, Mungu Musa anatangaza ujumber wa Mungu kwa Waisraeli. “Ikiwa mtasikiliza sauti yangu na kufuata agano langu mtakuwa watu wangu wa maana sana.” Mungu ana msimamo, na anatuita tumsikilize na kuzijali ahadi tulioweka naye wakati wa Ubatizo wetu. Mungu angetaka tuseme ukweli, tuwaheshimu wazazi wetu na tuhudhurie Misa Jumapili. Lakini badala ya kumsikiliza Mungu tunasikiliza sauti zingine. Wakati tuangukapo Mungu hutuonyesha kwamba anamsimamo, kwa sababu angetaku kuturudisha kwenye njia ya kweli na katika neema yake. Mtk Paulo kwenye Somo la Pili anatuonyesha kwamba wakati tulikuwa bado katika maasi yetu na Mungu, Mungu alituma Mwanae kutukomboa. Kama vile tunasikia kwenye Injili, Yesu aliona umati wa watu wakiwa na ulegevu wa kimwili na wa kiroho. Walikuwa kama kondoo bila mchungaji na bila kujua jinsi wangejipatia chakula cha kiroho. Tungesema kwamba barani Afrika twajikuta katika hali kama ile ya wakati wa Yesu. Hivi leo twaendelea kuvunja amri za Mungu na kutoitii Kanisa kama yule mtoto kwenye hadithi. Lakini Mungu katika Mwanae Yesu anatuonyesha msimamo wake na pia ana huruma. Anakuja kwetu kama yule baba alifanya kutuonyesha huruma wake na kutualika turudi katika neema yake. 

Ujumbe: 
1) Mungu ana msimamo na huruma kama yule baba kwenye hadithi; 
2) Mungu huzingatia tuisikilize sauti yake na sio sauti zingine; 
3) Wakati tulio katika maasi, Mungu hutuma Mwanae kama mchungaji kuturudisha katika neema yake.



Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment