“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Mei 4, 2023
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 13:13-25;
Zab 89:2-3,21-22,42:25,27 (K. 2);
Yn 13:16-20.
TUME BAHATIKA KUWA “WATUMWA”
“Nawaambieni, hakuna Mtumwa aliye mkubwa kuliko Bwana wake, na wala hakuna
mjumbe aliye mkuu kuliko yule aliye mtuma”. Yesu anajaribu kutuambia vitu
viwili. Cha kwanza, ni vizuri kujiona sisi wenyewe kama watumwa na wajumbe wa
Mungu na pili tunapaswa kumpa Mungu utukufu wote. Hili ni jambo muhimu la
kuishi katika maisha ya kiroho.
Kawaida habari ya kuwa “mtumwa” haitamaniki sana. Na kilicho kibaya kuhusu
utumwa ni kutendwa vibaya na Bwana wao. Wanatendwa vibaya na kuonekana kama
vitu tu tofauti na utu wao wa kibinadamu. Lakini chukulia hali nyingine ambapo
mmoja ni mtumwa alafu Bwana wake anampenda na jambo lake la kwanza kabisa la
Bwana huyu ni kumsaidia huyu “mtumwa” ili atambue talanta zake ili aweze
kukamilisha malengo yake ya maisha. Katika hali hii, “Bwana” huyu anamfanya
mtumwa kuwa na upendo na furaha na wala hata haribu utu wake wa kibinadamu.
Hali hii ndivyo ilivyo kwa Mungu. Hatupaswi kukataa habari ya kuwa watumwa
wa Mungu. Katika hali ya kweli, tunapaswa tutamani Mungu awe Bwana wetu zaidi
kuliko hata tunavyo tamani kuwa mabwana sisi wenyewe. Kwani Mungu atatutenda
vizuri zaidi kuliko hata sisi wenyewe. Kwani atatupa maisha ya utakatifu na
furaha na kwa unyenyekevu kutuweka katika mapenzi yake. Atatupa vyote tunavyo
hitaji kwa ajili ya kutenda yale anayo tuamuru. Kuwa “Mtumwa wa Mungu” ni kitu
kizuri na tunapaswa kutamani mpango huo katika maisha.
Sala: Bwana, ninajikabidhi katika kila unacho niamuru. Ninaomba mapenzi
yako yakamilike kwangu, mapenzi yako tu. Ninakuchagua wewe kuwa Bwana wangu
katika kila kitu na ninaamini upendo wako mkamilifu kwangu. Yesu, nakuamini
wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment