SIKU YA TATU, DOMINIKA
ROHO
MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME
Bwana
alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli; “Katika siku zile za mwisho asema Bwana,
nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, waume kwa wake,
watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota
ndoto….hata watumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika siku zile, nao
watautangaza ujumbe wangu. (Mdo.2:17-21)
Siku
ile ya Pentekoste, bada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa, mitume
waliwakumbusha watu maneno haya ya nabii Yoeli, na miaka mingi baadae, Petro
aliwaandikia barua Wakristu wa kwanza akawaambia; kila mmoja anapaswa kutumia
kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili mwema wa
zawadi mbali mbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya
Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu ili
katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye utukufu na
nguvu ni vyake milele na milele (Pet 4;10-11).
Mtaguso
wa Pili wa Vatikano ulitukumbusha jambo hilo hilo uliposema; “Roho Mtakatifu
anayetakasa taifa la Mungu kwa njia ya Sakramenti amewapa waumini mapaji ya
pekee na kumjalia kila mmoja kadiri apendavyo. Kwa hiyo kila mmoja amgawie
mwenzake kadiri ya vipawa alivyopewa, awe mgawaji mwaminifu wa neema ya Mungu,
alijenge kanisa zima katika upendo.
Tunao
wajibu wa kutumia vipawa tulivyojaliwa na Roho Mtakatifu kwa manufaa ya kanisa
zima, na kwa faida ya watu wote. Tuunganike sote pamoja na wachungaji wote
katika kazi hiyo ya utume. Tumuombe basi Roho Mtakatifu atusaidie kutumia vema
vipawa vyake alivyotujalia.
1. Ewe Roho Mtakatifu uwape wakristu neema
na nguvu za kutumia vema vipaji ulivyowajalia kwa ajili ya kujenga kanisa lako
popote duniani, kwa ajili ya wokovu wa watu wote
W. Twakuomba utusikie
2. Utujalie sisi sote mapaji yako saba,
tupate kukutumikia kwa uchaji
W. Twakuomba utusikie
3. Utujalie tuwe mitume wa kweli wa
wenzetu, tushirikiane na wachungaji wetu katika huduma za kuwaongoza watu wote
na kuwafikisha mbinguni
W. Twakuomba utusikie.
4. Utujalie hekima na nguvu za kuwahudumia
watu wote kwa mapendo ya kweli yasiyo na kinyume
W. Twakuomba utusikie
5. Utujalie neema ya kumpenda Mungu kwa
moyo wote na kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe
W. Twakuomba utusikie
6. Utupe neema ya kulisikia neno lako na
kulifuata, nayo mawazo yetu na matendo yetu yafuate daima mwongozo wako
mtakatifu
W. Twakuomba utusikie
7. Uwazidishie mapaji yako wale wote
wanaotumia vyema vipawa vyao, uwarudishe na wale wanaotumia vibaya rehema zako
W. Twakuomba utusikie
TUOMBE:
Ewe
Roho Mungu ndiwe uliyewapa waumini vipawa vyako kwa kadiri unavyotaka. Utujalie
tuyapokee na kuyatumia vyema mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina
lako na kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu
Bwana wetu.
No comments:
Post a Comment