“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumapili, Aprili 30, 2023
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 2: 14, 36-41;
Zab 23: 1-6;
1 Pet 2: 20-25;
Yn 10: 1-10.
KUKUTANA NA MCHUNGAJI MWEMA!
Jumapili ya nne ya Pasaka inajulikana kama jumapili ya Mchungaji Mwema,
kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji mwema”. Yesu anatupa
sura ya Mchungaji mwema anaye wafahamu kondoo wake: anawaita, anawalisha na
kuwaongoza. Ni kwasababu ya hili Kanisa limeipendekeza kuwa siku ya kuombea
miito duniani.
Yesu anaonesha wazi tofauti ya wachungaji. Tofauti anayotoa ni juu ya
mchungaji yule anaye wafahamu kondoo wake na kuwajali, na wale wanaofuata tu
mkumbo bila sadaka ya upendo. Yesu alitolea sadaka kamilifu kama Mchungaji wa
Kimungu. Alikuwa yupo tayari kutembea nasi katika njia zote, sisi kondoo wake.
Alikuwa yupo tayari kutoa sadaka ya kila kitu. Hakutaka mateso, kuonewa,
kukataliwa na mambo mengine yamuondoe kutoka katika lengo lake la kuwajali na
kuwatunza watu wake katika njia kamili. Inapaswa ituguse na sisi, kutufariji na
kutupatia sisi ujasiri na kutambua ni kwa jinsi ghani upendo wake ulivyokuwa
mkubwa kwetu.
Wakati upendo aliotoa mmoja kwa ajili yetu ni kamili, tena wakati wa wakati
mgumu, huu ni msaada mkubwa. Na upendo unaotolewa kwa mwingine kama huu
unatengeneza muunganiko wa kiroho ambao ni imara kuliko matatizo tunayo weza
kukutana nayo. Haijalishi ni kitu ghani kigumu kinachoweza kuja katika njia
zetu, tunapaswa kutambua upendo na msaada usio na kikomo kutoka kwa Mchungaji
wetu mwema. Na kama tunaweza kuona upendo huo kamili kutoka kwa wengine,
tunakuwa kweli tumebarikiwa mara mbili. Katika hali nyingine Yesu anaongea
kuhusu mfano wa mtu mwingine ambaye sio mchungaji mwema, ambaye anaona mbwa
mwitu wakija na yeye hukimbia. Tunapaswa kuona ndani ya mtu huyu, vishawishi
vyote ambavyo vyaweza kuja katika maisha yetu. Ni vigumu kubaki wakati wa
nyakati ngumu. Ni vigumu kuwa karibu na wale wenye shinda wanapo tuhitaji sisi.
Ni vigumu kuwa waminifu mpaka mwisho bila kuwa na aibu tunapo kutana na
vishawishi vya hofu. Yesu anatupa nguvu na msaada wa upendo kamili yeye akiwa
kama Mchungaji wetu mwema, lakini pia anatuhitaji nasi turudishe upendo huu huu
kwake, kwa kuwapatia wengine upendo huu huu mkamilifu. Pale ulipo shindwa na
kupungukiwa tunamuomba yeye akuchunge kama mchungaji ili nawe uweze kuwachunga
wengine. Mkimbilie mchungaji mwema na amini upendo wake kwako.
Leo, Kanisa zima linatukumbusha hitaji letu la kuomba, kama Yesu mwenyewe
alivyo waambia wanafunzi wake, hivyo kwamba "mwombeni Bwana wa mavuno
apeleke watenda kazi katika mavuno yake" (Lk 10: 2). Tangu hapo awali
Kanisa “ kwa asili yake ni umisionari" (Ad Gentes, 2), wito wa Ukristo
unazaliwa ndani ya watu kutokana na kazi ya umisionari. Kusikia na kufuata
sauti ya Kristo Mchungaji mwema, maana yake ni kuruhusi tuvutwe naye na
tuongozwe naye, kujiweka wakfu kwake maana yake kumruhusu Roho Mtakatifu
kututumia sisi katika mabadiliko haya ya umisionari, na kuamsha ndani yetu
tamaa, furaha na ujasiri wa kutoa maisha yetu wenyewe katika utumishi wa Ufalme
wa Mungu.
Katika mzizi wa kila wito wa Kikristo tunaona harakati hii ya msingi, ya
kuacha nyuma faraja yetu na mambo yote yanayo tupendezesha nafsi zetu na
kujikita katika maisha ya Yesu Kristo. Ina maana ya kuondoka, kama Abrahimu, na
kuacha sehemu yetu ya asili na kwenda mbele kwa uaminifu, tukijua kwamba Mungu
atatuonesha njia ya nchi mpya. Hii "kwenda mbele" isi tazamwe kama
ishara ya mpango tu wa maisha ya mtu binafsi, hisia ya mtu, utu wa mtu
mwenyewe. Kinyume chake, wale ambao wanamfuata Kristo wanapata uzima kwa wingi
kwa kujiweka wenyewe bila kujibakiza katika utumishi wa Mungu na ufalme wake.
Wito wa Kikristo kwanza kabisa ni wito wa upendo, upendo ambao hutuvuta sisi na
kutuelekeza nje ya sisi wenyewe. Kuitika wito wa Mungu, maana yake kumruhusu
yeye atusaidie kujiacha wenyewe kwakuondokana na usalama wetu wa uongo, na
kutoka nje na kuenenda kwenye njia inayo ongoza kwa Yesu Kristo, aliye asili na
hatima ya maisha yetu na furaha yetu.
Katika siku hizi kwanza tunaombwa tuombee Kanisa liweze kupata wachungaji
wema na waadilifu wa kufanya kazi ya Kristo ya kueneza Injili, na kwamba Kanisa
liweze kupata vijana wengi wanoitwa kwenye wito wa upadre na utawa ikiwa ni
pamoja na watoto wetu wenyewe.
SALA: Baba wa huruma, uliyemtoa mwanao kwaajili ya wokovu wetu na ambaye
anatutia nguvu kila wakati kwa zawadi ya Roho wako, tujaliye sisi jumuiya ya
Wakristo tulio hai, upendo na furaha, vilivyo vya muhimu kwa maisha ya kindugu,
na vinavyojenga ndani ya wadogo mwamko wa wito wakujitoa wenyewe wakfu kwako na
kwaajili ya wito wa uenezaji wa neno lako. Dumisha ndani ya jumuiya hizi
majitoleo ya kutoa katekesi ya kuitika wito huu wakujitoa wakfu kwako .
Wajaliye hekima inayohitajika katika maamuzi ya kufuata wito wako, ili katika
yote ukuu wa huruma yako ya upendo iweze kungara. Tunaomba Maria, Mama na
uliyekuwa kiongozi wa Yesu, utombee. Yesu tunakutumainia wewe. Amina
No comments:
Post a Comment