MASOMO
YA MISA, MACHI 30, 2023
ALHAMISI, JUMA LA 5 LA KWARESIMA
SOMO 1
Mwa. 17:3-9
Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia,
akasema, Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani
nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami
nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. Agano langu nitalifanya
imara katia ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa
agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako, na
vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako
baada yako, nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa
ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano
langu, wewe na uzaqo wako kwa vizazi vyao baada yako.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 150: 4-9 (K) 8
(K) Analikumbuka agano lake milele.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake siku zote.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. (K)
Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake. (K)
Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka. (K)
SHANGILIO
2 Kor. 6:2
Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa, tazama,
siku ya wokovu ndiyo sasa.
INJILI
Yn. 8:51-59
Yesu aliwaambia Wayahudi: Amin, amin, nawaambia,
Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia,
Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu na manabii wamekufa; nawe wasema,
Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu
Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Yesu akajibu, nikijutukuza mwenyewe, utukufu
wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu
wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui,
nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu,
baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona,
akafurahi.
Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado
miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu
akajificha, akatoka hekaluni.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment