“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumapili, Aprili 9, 2023
VIGILIA YA PASAKA
Mwa 1:1-2:2, Zab 103:1-2,5-6,10,12-14,24,35 au Zab 32:4-7,12-13,20,22;
Mwa 22:1-18, Zab 15:5,8-11;
Kut 14:15-15:1, Kut 15;
Isa 54:5-14 Zab 29:2,4-5,11-13;
Isa 55:1-11, Is 12;
Bar 3:9-15,32-4:4, Zab 18:8-11;
Ez 36:16-28, Zab 41:2-3,5,42:3-4 au Zab 50:12-15,18-19;
Rom 6:3-11, Zab 117:1-2,16-17,22-23;
Mt 28:1-10.
KUFANYWA UPYA KWA NJIA YA KRISTO!
Liturjia ya leo inatualikwa kwenye mafumbo ya uumbaji mpya. Moto mpya
unawasha na mshumaa mpya wa Pasaka unawashwa. Kanisa linasogea kutoka kwenye
giza kuelekea kwenye mwanga tunavyo washa mishumaa yetu kutoka katika moto huu.
Maji mapya yanabarikiwa na kwa maji hayo waumini wapya wanaingia katika kanisa
kwa njia ya ubatizo. Ndio, Yesu anafanya mambo yote mapya.
Maadhimisho yana anza wakati taa zote zikiwa zimezimwa. Padre anabariki
moto na kuandaa mshumaa wa Pasaka. Moto unatumika kuwasha mshumaa unaotumika
kama mwanga alama ya Yesu. Mwanga umetajwa katika Biblia katika msatari wa tatu
wa sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo: Mungu anasema “na kuwe na Mwanga”.
Kabla ya hili mwandishi anaonesha uwepo wa giza kubwa linalotisha. Mshumaa wa
Pasaka unatukumbusha sisi kuhusu Mwanga. Sisi wote tumetembea katika giza Isaya
anasema 9:2. Mioyo yetu ilivyokuwa katika giza ilikwama (Yn 11:10). Hatukujua
tuende wapi wala tupo wapi hadi tukaanguka kwenye dhambi.
Yesu, Mwanga wa ulimwengu (Yn 9:5) alikuja ulimwenguni kuja kuuangaza
ubinadamu wetu (Yn 1:4) na bado wakakataa mwanga huu na watu wakapenda mno giza
(Yn 3:19). Usiku huu wa Pasaka unatukumbusha kuhusu hili. Jengo la Kanisa lipo
katika giza. Tupo gizani kama hatuna Kristo. Licha ya hili giza kubwa mwanga
mdogo wa mshumaa huu wa Pasaka unauwezo wa kutuangaza nasi tukaona mlango wa
kuingia kanisani. Mwanga huu mdogo unatusaidia kuingia bila kujikwaa. Watu
walivyo washa mishumaa wao kutoka katika mshumaa wa Pasaka, mwanga umeangaza
zaidi na zaidi tukaanza kuona nyuso za kila mmoja wetu. Mwanga wa Kristo
unafufua sura ya Mungu ndani yetu. Mwanga tunaopokea haupaswi kufichika, na
wala hatupaswi kuanguka kwenye giza, kwani sisi sasa tumekuwa watoto wa mwanga
(1 Thes 5:5).
Tunapaswa kwenda ulimwenguni na kuangazia kama nyota ya mbinguni inavyo
angaza kwenye anga. Licha ya kuwa ndogo kwa muonekano inangaa kati ya giza
kubwa lililopo angani. Maisha yetu ya Ukristo yanapaswa kuwa shahidi wa Kristo.
Mwanga wetu tunaopokea kwa Kristo haupaswi kungara sana kiasi cha kuwaumiza
wengine. Na wala haupaswi kuwachoma kiasi cha kuwaachia makovu. Tunapaswa kuwa
wanyenyekevu na kuwakilisha mwanga wa Kristo kwa mapendo. Yesu ni mwanga
unaoendelea kungaa katika ulimwengu huu wa giza. Amefufuka na yupo pamoja nasi
na atakuja siku ya mwisho. Tutumie muda wetu tukiwa hapa duniani kwa kuleta
mwanga wa Kristo ulimwenguni.
Yesu anaumba upya ulimwengu uliokuwa umeanguka na kuharibiwa na dhambi na
anatuumba upya kila mmoja wetu. Analeta uponyaji na utakatifu katika maisha
yetu. Hatuwekei viraka bali anatufanya wapya kabisa. Tunamuomba yeye atujaze na
furaha za ukombozi wake. Tunamuomba aweke wimbo mpya mioyoni mwetu. Wewe ni
kiumbe kipya.
Sala: Bwana nifanye mpya: nijaze na mwanga wako na fukuza giza ndani
mwangu. Nitoe katika kifo na kunipeleka katika uhai, kutoka katika mtafaruku na
kuniweka kwenye njia njema, kutoka katika giza kwenda kwenye mwanga. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
TUNAWATAKIA HERI YA PASAKA WASOMAJI WA TAFAKARI ZETU NA MARAFIKI
WOTE -Furaha ya Kikatoliki- KRISTO AWAANGAZEE. AMINA
No comments:
Post a Comment