“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatano, Aprili 5, 2023
Juma Kuu
Isa 50: 4-9;
Zab 68: 8-10, 21-22, 31, 33-34;
Mt 26: 14-25.
KUBEBA MISALABA YETU!
“Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu;
sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate." Mstari huu kutoka
kitabu cha nabii Isaya unatukumbusha juu ya uchungu wa Yesu. Lakini, tunaweza
kufikiria tu kile alichokihisi Yesu aliposoma maneno haya ya Isaya. Je,
unafikiri maneno haya yalimpelekea awe na hofu? Au labda kwa sababu yeye
alikuwa mwana wa Mungu, jambo hili halikumsumbua yeye kabisa? Pangine ukweli
upo sehemu fulani kati ya hayo. Kuwa binadamu, Yesu kiasili alihisi matatizo
makubwa juu ya kile kilichokuwa kikimngojea yeye. Lakini katika Umungu wake,
aliweza kutamka kwa kujiamini sana, Bwana Mungu ndiye msaada wangu hivyo sina
mashaka. Hivyo hakika alikuwa na hofu kubwa juu ya majaribu yaliopo mbele yake,
vilevile Yeye alijawa na nguvu akijua kuwa Baba yake alikuwa pamoja naye na
kamwe asinge mwacha.
Kuna uwiano hapa kwa maisha yetu. Hatuwezi kuona wakati ujao, lakini
tunatambua kuwa tuna ugumu fulani waweza kuja katika maisha yetu na tunapaswa
kuushughulikia. Pengine hatupo katika hali ambayo dhambi yetu inatuonesha tuna
mkana Yesu moja kwa moja, lakini kila mmoja anaweza kuona aina fulani ya dhambi
katika maisha yake. Tumia juma hili kwa uaminifu na kweli. Huruma ya Mungu ni
ya ndani sana na njema mno, kiasi kwamba ungeielewa, kusingekuwa na haja ya
kubaki na dhambi zako ukifikiria niungame namna ghani. Hali halisi haipo kama
tunavyo ifikiria sisi wenyewe. Kama Yesu, tunajikabidhi kwa upendo na msaada wa
Baba yetu wa Mbinguni. Tukiwa naye, ni hakika kwamba tunashinda tatizo lolote
lile, kwani hawezi kuwatupa watoto wake.
Sala: Bwana, ninaomba unisadie katika juma hili niweze kukabili dhambi
zangu na udhaifu wangu. Mimi ni mdhambi, Bwana mpendwa, lakini inaweza kuwa
vigumu sana kwangu kukubali ukweli huu. Ninaomba nikabidhi dhambi zangu kwako,
ili niweze kuwa huru, na kupokea nafasi katika huruma yako kuu. Yesu, nakuamini
wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment