MASOMO YA MISA, MACHI 20, 2023
JUMATATU, JUMA LA 3 LA KWARESIMA
SHEREHE YA MT. YOSEFU, MUME WA BIKIRA MARIA
SOMO 1
2Saw. 7: 4 – 5, 12 – 14, 16
Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia
Nathani kusema, Enenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, Bwana asema hivi, siku
zako zitakapo timia, ukalala na Baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako,
atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye
atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake
nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu,
akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo yako, na ufalme wako, vitathibitishwa
milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 89:1 – 4, 26, 28 (K) 36
(K) Wazao wake watadumu milele.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote
uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. (K)
Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemwapia Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele. (K)
Yeye ataniita, Wewe baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Hata milele nitamwekea fadhili zangu,
Na agano langu litafanyika amini kwake. (K)
SOMO 2
Rum. 4:13, 16 – 18, 22
Ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu
alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa
Imani. Kwa hiyo ilitoka katika Imani, iwe njia ya neema, ili kwamba ile ahadi
iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila kwa wale wa Imani ya
Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba
wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha
wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza
kutarajiwa, ilia pate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo
utakavyokuwa uzao wako. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Zab. 84:5
Heri wakaao nyumbani mwako, Ee Bwana.
INJILI
Mt. 1:16, 18-21, 24
Yakobo alimzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa
yesu aitwaye Kristo.
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi.
Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana,
alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile
alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha malaika wa Bwana
alimtokea katika ndoto, akimchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza
wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye
ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya
kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment