NJIA YA MSALABA FUPI
Jinsi inavyotumika na Mapadre Wafrasiskani katika Misioni zao.
Kituo cha kwanza:
Yesu anahukumiwa kifo:
Ee Yesu mnyenyekevu na usiyelalamika nifundishe mimi niyakubali majaribu.
Kituo cha pili:
Yesu anabeba msalaba wake:
Yesu wangu, Msalaba huu, ulitakiwa uwe wangu, sio Wako; dhambi zangu zilikusulubisha Wewe.
Kituo cha tatu:
Yesu ananguka mara ya kwanza:
Ee Yesu, kwa kuanguka mara hii ya kwanza, kamwe usiruhusu nianguke katika dhambi ya mauti.
Kituo cha nne:
Yesu anakutana na Mama Yake:
Ee Yesu, kamwe mahusiano ya kibinadamu, hata yawe mazuri kiasi gani, yasinizuie Kufuala njia ya Msaiaoa.
Kituo cha tano:
Simoni wa Kirene anamsaidiia Yesu kubeba Msalaba:
Simoni bila kutaka, alikusaidia Wewe; kwa uvumilivu niteseke yote Kwa ajili yako.
Kituo cha sita:
Veronika anapangusa Uso wa Yesu:
Ee Yesu, Wewe uliyechapa Sura Yako Takatifu kwenye Kitambaa cha Veronika, Uichape pia bila kufutika juu ya Moyo wangu.
Kituo cha saba:
Yesu anaanguka mara ya pili:
Kwa kuanguka mara hii ya pili, unilinde Ee Bwana mpendwa dhidi ya kuanguka tena katika dhambi.
Kituo cha nane:
Yesu anatuiiza Wanawake wa Yerusalem:
Faraja yangu kuu itakuwa nikusikia Wewe ukisema: "Dhambi zako nyingi zimesamehewa, kwa sababu wewe ulipenda zaidi".
Kituo cha tisa
Yesu anaanguka mara ya tatu:
Ee Yesu wakati wa uchovu wa safari ndefu ya maisha, Uwe nguvu yangu na bidii yangu.
Kituo cha kumi:
Yesu anavuliwa nguo Zake:
Roho yangu imeporwa vazi lake la Usafi; Ee Yesu mpendwa, nivishe kwa vazi la toba na malipizi.
Kituo cha kumi na moja
Yesu anasulubishwa Msalabani:
Wewe unawasamehe adui zako; Ee Mungu wangu, unifundishe nami nisamehe majeraha na kuyasahau.
Kituo cha kumi na mbili:
Yesu anakufa Msalabani:
Yesu wangu, Wewe unakufa lakini Moyo wako Mtakatifu bado unadunda kwa mapendo kwa ajili ya Wanao wadhambi.
Kituo cha kumi na tatu:
Yesu anashushwa kutoka Msalabani:
Ee Mama mwenye uchungu mwingi, nipokee mimi katika mikono Yako, na nijalie niwe na majuto ya dhati kwa dhambi zangu
Kituo cha kumi na nne:
Yesu anazikwa kaburini:
Wakati ninapokupokea ndani ya Moyo wangu katika Komunio Takatifu, Ee Yesu unifanye niwe mahali panapofaa kwa ajili ya mwili Wako Mwabudiwa. Amina.
Kabla ya kila kituo:
K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru;
W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.
Baada ya kila kituo:
'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba',
K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie!
K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina
No comments:
Post a Comment