ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Januari 8, 2023
Sherehe ya Tokeo la Bwana (Epifania)
Isa 60: 1-6;
Zab 72: 1-2, 7-8, 10-13;
Efe 3: 2-3, 5-6;
Mt 2: 1-12.
ZAWADI KWA DUNIA NZIMA!
Katika somo la kwanza, katika ono lake la
kinabii, Isaya anaona ujio wa Mungu ulimwenguni. Utakuja muda ambapo watu wote
wataletwa pamoja mbele ya Bwana na watabarikiwa sana. Utukufu wa Bwana utashuka
ulimwenguni na utukufu wake utauzunguka uumbaji wote.
Tukio hili takatifu litalibadilisha jiji la
Yerusalemu na wale wote wanaofanya kazi na kuvumilia watapokea mwanga wa uhai.
Katika somo la pili, Paulo anaifumbua siri
ambayo Mungu anaitoa kwa utukufu wake watu wote pamoja na wapagani, kuwafanya
warithi wa ufalme wake. Anasema “sasa imefunguliwa kuwa wapagani wanashiriki
urithi ule ule”. Ukombozi wa ulimwengu, Mungu pia anawapenda wasio Wakristo
kwani wao pia ni wapokeaji.
Leo tunasherehekea sherehe ya Tokeo la Bwana. Ni
sherehe ya dhihirisho la Bwana wetu kwa watu wa Mataifa. Kulikuwa na mamajusi
watatu kutoka mashariki waliokuja kwa Mfalme mpya aliyezaliwa. Mamajusi hawa,
watu wa mataifa, ambao hawakuwa katika utajiri wa pamoja wa Waisraeli, walikuwa
ni watu waliosoma nyota kwa lengo la kubaini siri na ujumbe wake. Walipokuja
katika mahakama ya mfalme, walimuuliza Herode, yuko wapi mfalme wa Wayahudi
aliyezaliwa? Hawakuuliza kama mfalme wa wayahudi amezaliwa? Walikuwa na uhakika
kuwa mfalme alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa tu hawana uhakika wa sehemu yake
alipozaliwa, bali juu ya ukweli kwamba amezaliwa walikuwa nao.
Kama tu vile Yeye alivyo jidhihirisha Yeye
Mwenyewe kwa wale mamajusi, kila siku Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwetu sisi
katika Ekaristi Takatifu. Tunamtukuza Yeye, tunamshukuru na kumfanya yeye
afahamike ulimwenguni kote. Basi tujitoe sisi wenyewe kama zawadi na tuunganike
naye na kuhubiri:Mungu amejidhihirisha mwenyewe duniani. Yesu
anajitoa mwenyewe zawadi kwa dunia nzima.
Sala: Bwana, niwezeshe niweze kujitoa Mimi
mwenyewe kama zawadi kwako. Amina..
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment