“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Januari 26, 2023
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Watakatifu Timotheo na Tito(Maaskofu)
2 Tim 1: 1-8 au Tit 1: 1-5;
Zab 96: 1-3, 7-8, 10;
Lk 10: 1-9.
WAJUMBE WA AMANI
Leo tunaangalia juu ya wazee wetu wa Imani na jinsi walivyo weka Injili
katika matendo yao baada ya ufufuko wa Yesu. Hawa wanaume na wanawake ni wa
kizazi cha pili: wafuasi wa wafuasi na walikuwa wakitumwa mara kwa mara wakiwa
wawili wawili kuhubiri kwa uwepo wao. Kwa njia ya kutembelea na kusafiri
inaonyesha kwamba ufalme wa haki na Amani ulikuwa tayari Ulimwenguni.
Ujumbe kutoka katika barua kwa Timotheo, Paulo anaelezea mapendo yake
makubwa kwa Timotheo, na wenzake katika utume, na hamu yake kubwa ya kumuona.
Anamshukuru Mungu kwa Imani ya Timotheo alioonesha kwa mama yake Myahudi na
bibi yake Loisi. Wakati huo huo anamkumbusha Timotheo kuhusu zawadi aliopokea
wakati Paulo alivyo mwekea mikono juu yake. Zawadi anayosema Paulo, ilikuwa sio
ya woga bali yenye nguvu, upendo na ujasiri na kuleta ujasiri wote wakuhubiri
Injili hata wakati, wa kipindi cha Paulo, kuonewa na kuteswa. Katika somo la
kuchagua la pili, kutoka katika barua ya Paulo kwa Tito, Paulo anawakumbusha
wamisionari wenzake juu ya kazi ya mtume. Ni “kuwaleta wote ambao Mungu
amewachagua kwenye Imani na akili ya kweli inayo ongoza kwenye dini ya kweli”.
Katika somo la Injili linaongelea kuhusu maelekezo anayotoa Yesu kwa wale
Wafuasi 72 anavyowatuma kwenda kwa utume kufanya kazi ile ile aliokuwa akifanya
yeye mwenyewe. Maneno yake ya ufunguzi ni kweli kama ilivyokuwa katika kipindi
cha Timotheo na Tito: “mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache; hivyo
muombeni Bwana wa mavuno apelike wafanya kazi katika shamba lake.” Ujumbe wao
ulipaswa kuwa wenye kuponya. Sio tuu uponyaji wa mwili tu, bali uponyaji wa
kila aina unaofanya mahusiano na maisha ya watu yalete Amani. Kwa kufanya hivi
walileta uwepo wa ufalme wa Mungu kwa watu walio watembelea. Ni upendo na uwezo
wakuishi kwa pamoja kwa kujaliana na kusaidiana vinaonesha uwepo wa Ufalme wa
Mungu katika maisha yetu. Haya ndio Timotheo na Tito walijitolea kufanya.
Sisi-hata tungekuwa na cheo ghani katika jamii ya Kikristo-tunaitwa kufanya
hayo hayo.
Sala: Bwana, ninaomba niwe mjumbe wako wa Amani na uponyaji. Ninaomba
nijifunze kutegemea nguvu zako na kuishi maisha nikijikabidhi katika utume
wako. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment