Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

UBATIZO, UHAI MPYA WA NEEMA.


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu, Januari 2, 2023
Juma kabla ya Epifania

Kumbukumbu ya Watakatifu Basili Mkuu na Gregori Nazienzi

1 Yoh 2:22-28;
Zab 98: 1-4;
Yn 1:19-28.


UBATIZO, UHAI MPYA WA NEEMA.

Yohane alisema “Ninabatiza kwa maji”. Ubatizo wa Yohane ulikuwa tofauti na ubatizo wa Yesu. Yohane anaelezea tofauti ni hii: “Mimi nabatiza kwa maji kuonyesha kuwa mmetubu, yule ajaye nyuma yangu, atawabatiza kwa Roho Mtakatifu”. Ubatizo wa Yohane ulikuwa tu ni ishara ya kutubu. Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni sakramenti ya kuzaliwa tena. Ubatizo wa Yohane unaashiria kutubu kutoka katika maisha ya dhambi. Ubatizo wa Yesu unaashiria ukaribisho wa maisha mapya ya neema: Maisha ya Yesu mfufuka ambayo watu hawayaelewi. Je, ni namna gani njema ninavyoboresha maisha yangu mapya?

Sala: Bwana, Nisaidie niwe mpya ndani ya Roho Mtakatifu. Amina.

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment