MASOMO YA MISA, JANUARI 11, 2023
JUMATANO, JUMA
LA 1 LA MWAKA WA KANISA
SOMO 1
Ebr. 2:14-18
Kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeyey
naye vivyo hivyo alishiriki yay ohayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye
aliyekuwa na nguvu za mauti, ayani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba
maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.; maana ni
hakika, hatwai asili ya malika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo
ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu
mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za
watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao
wanaojaribiwa.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 105:1-4, 6-9 (K) 8
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
Mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote. (K)
Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana,
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake siku zote. (K)
Enyi wana wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo wateule wake.
Yeye Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake. (K)
Analikumbuka agano lake milele,
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka. (K)
SHANGILO
Efe. 1:17, 18
Aleluya, aleluya,
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya
hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
INJILI
Mk. 1:29-39
Siku ile, Yesu alipotoka katika sinagogi,
walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohane. Naye mkewe
Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia
habari zake. Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha,
akawatumikia.
Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa,
walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa
umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa
pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka
akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe
wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia,
Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko
nako; maana kwa hiyo nalitokea. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika
nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora
- Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are
published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings
are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment