“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Desemba 10, 2022
Juma la 2 la Majilio
YbS 48: 1-4, 9-11;
Zab 79: 2-3, 15-16, 18-19;
Mt 17: 10-13
KUKUBALI KUTUBU
Kazi ya Yohane Mbatizaji kama Elisha aliyekuja
Waandishi walishindwa kuiona. Walishindwa kumuona yeye akitimiza kazi ya Elisha
ya kuandaa njia kwa ajili ya Bwana. Kama Yohane alivyokuwa na kazi ya pekee ya
kumtambulisha na kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa Kristo, sisi pia tuna kazi
ya kumkaribisha Yesu daima. Yesu alikuja miaka mingi iliopita, lakini daima
anatamani kuja daima katika maisha yetu. Na anaweza kuja tu kama tumejiandaa
vizuri.
Ujumbe mkuu wa Yohane ni kutubu dhambi zetu.
Ingawaje sisi wote tunakazana kujikinga na dhambi, kwasababu ya matokeo ya
kuanguka kwa Mwanadamu, hatupaswi kusahau kwamba wito wetu ni kuwa wakamilifu,
kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu. Tunaitwa kutambua
dhambi zetu, kuziungama, na kujitahidi kujinasua kutoka kwenye dhambi hizo.
Kipindi cha majilio ni kipindi muhimu cha kufanya
hivyo daima, na ni muhimu kutafuta neema zinazopatikana kwa neema ya Sakramenti
ya kitubio katika kipindi hiki kitakatifu. Tujitazame wenyewe katika mioyo yetu
ni kwa jinsi ghani tulivyo tayari kuihubiria mioyo yetu kuhusu kutubu na kuacha
dhambi. Kukubali toba kutubu kipindi hiki ni kitu chema kabisa ambacho twaweza
kufanya ili kuandaa kuja kwa Kristo daima katika maisha yetu.
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuziona dhambi zangu
kadiri tunavyozama katika kipindi hichi cha majilio. Nisaidie niweze kutambua
yale yote yanayonifanya niwe mbali nawe na kuyaacha kwa moyo wote. Yesu
nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment