Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUITIKA NAKUTOA JIBU KWA NENO LA MUNGU!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Desemba 31, 2022
Oktava ya Kuzaliwa Bwana

1 Yoh 2: 18-21;
Zab 96: 1-2, 11-13;
Yn 1: 1-18


KUITIKA NAKUTOA JIBU KWA  NENO LA MUNGU!


Dibaji ya Injili ya Yohane ni nyimbo nzuri inayoimba juu ya simulizi ya Krismasi/Noeli fumbo la Umwilisho. Kutoka katika ufahamu huu wa binafsi wa kuishi na Kristo, Yohane alikuwa ameshawishika kwa kina sana kuwa Yesu ndiye Neno, Aliyekuwako tokea mwanzo pamoja na Mungu, Aliyekuwa mwili na kukaa kwetu. Andiko hili tukufu linatoa muunganiko wa imani ya Kikristo. Ukristo sio dini ya kitabu bali ni dini au neno la Mungu, sio neno lililoandikwa na lisilo nena, bali ni ya umwilisho na Neno liishilo. Kwahiyo, hususani katika Adhimisho la Ekaristi, wakati habari njema inapohubiriwa, ni Kristo Mwenyewe ndiye anayehubiri kupitia watumishi wake, wakitafuta jibu sawa la imani ipendwayo ambayo Yeye aliomba kwa wale wote ambao Aliwahubiria katika Palestina. Na kanisa ni katika kiini chake cha ndani, jumuiya ya wale wote wanaosikia neno la Mungu na kulizingatia. Swali ni, je, kama wanajumuiya wa hii jumuiya ya imani inayosikiliza, je, ni namna gani tunajibu?  Je, daima tupo tayari kujifungua wenyewe katika neno la Mungu namapenzi yake kwetu sisi? Au tunajikuta sisi wenyewe hatupendi, tusio badilika kutokana na nguvu ya neno la kubadilisha, isiyoenda kutokana na tofauti ya neema iletwayo?

Sala: Bwana, tuongoze katika upendo mkuu wa neno lako na tutie nguvu ya unyenyekevu katika kujibu na kutii imani. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment