Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KATIKA MIGUU YA FAMILIA TAKATIFU YA NAZARETI


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Desemba 30, 2022
Oktava ya Kuzaliwa Bwana.

Sikukuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu

YbS 3: 2-6; 
Zab 127: 1-5; 
Kol 3: 12-21; 
Mt 2: 13-15, 19-23

KATIKA MIGUU YA FAMILIA TAKATIFU YA NAZARETI

Sikukuu ya familia takatifu ni sikukuu ya kila familia ya Kikristo. Liturujia inatualika sisi kuiunda familia yetu kutokana na mfano wa familia takatifu ya Nazareti. Sisi sote tumezaliwa na tumelelewa katika familia. Katika sherehe ya familia takatifu tutajaribu kutafakari  juu ya umuhimu na utume wa familia ya Kikristo.

Baba, mama na watoto wanaunda familia, kila mmoja wa familia anathamani, anapaswa apendwe na mtu aheshimiwe. Ukamilifu wa maisha ya kifamilia unaonekana katika familia takatifu ya Nazareti. Katika familia hii tunamuona, Yosefu ambaye daima alikuwa makini kuisikiliza sauti ya Mungu, Maria aliyekuwa daima tayali kuyafanya mapenzi ya Mungu na Mtoto Yesu daima aliwatii wazazi. Ulikuwa ni muungano wa watu tofauti tofauti. Je, familia zetu zinaishi katika umoja au zinaishi tu pamoja kwa sababu ya uhitaji?

Misingi muhimu ambayo inaunda familia ni upendo na uhai. Kila mwanafamilia anamuendeleza mwanafamilia mwingine kwa upendo. Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wanashirikisha upendo na uhai wao kwa viumbe vyote, hususani kwa wanadamu. Yesu alishirikisha upendo huu na uhai kwa familia yake mwenyewe ya Nazareti, pamoja na Yosefu na Maria na pamoja na wandamu wote. Je, ni kiasi gani cha uhai na upendo ninachokitoa katika familia yangu mwenyewe?

Familia ni Kanisa la nyumbani. Linawakilisha Kanisa katika ngazi ya familia. Kitu cha muhimu zaidi ambacho familia inahitaji ni sala ya familia. Kadiri tulivyosikia mara nyingi, ‘familia inayosali pamoja huishi pamoja’.  Inapata nguvu na virutubisho vya kuishi kwa njia ya sala tu. Je, ninaingia nyumbani kwangu kana kwamba ninaingia Kanisani?

Sala: Yesu uliishi ndani ya familia yako Nazareti, tembelea familia yangu leo ili uifanye iwe yako.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment