“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, Novemba 6, 2022
Juma la 32 la Mwaka C wa Kanisa
2 Mak 7:1-2, 9-14;
Zab 16: 1, 5-6, 8, 15;
2 The 2:16-3:5;
Lk 20:27-38.
MBINGUNI NI HAKIKA!
Katika Injili ya leo tunawaona Masadukayo
wakijaribu kumtega Yesu kwa maswali kuhusu swala la ndoa na maisha baada ya
kifo. Hili linafuata mtiririko wa Mafarisayo kutaka kumtega Yesu kwa kuleta
swala juu ya kulipa kodi kwa Kaisari. Yesu anajibu hali zote katika hali ya
urahisi kabisa.
Masadukayo walikuwa ni kikundi cha dini katika
jumuiya ya Wayahudi. Walikuwa ni tofauti na Mafarisayo na walikubali vitabu
vitano tu vya Biblia (Tora) na hawakukubali kuamini uwepo wa vitu kama Malaika,
maisha baada ya kifo nk. Huku wakitaka kumtega Yesu walileta habari ya mwanamke
na ndugu saba waliomuoa mwanamke huyo mmoja baada ya mwingine ili kutimiza
sheria za Walawi za Kiyahudi kwamba mwanamume anapaswa kuoa mwanamke mmjane
asiye na mtoto ili ampatie watoto ndugu yake aliyekufa bila mtoto. Swali ni
kwamba, huyu mwanamke atakuwa wa nani katika maisha yajayo?
Jibu la Yesu lina sehemu mbili: kwanza, maelezo
ya kufikirika kuhusu maisha yajayo na pili kuboresha jibu lake kutoka katika
Tora (kwasababu Masadukayo waliamini Tora tu). Katika sehemu ya kwanza ya jibu
la Yesu, anatofautisha sifa za maisha ya ulimwengu huu(duniani) na sifa za
ulimwengu ujao (mbinguni) ili kurekebisha wanapokosea Masadukayo. Masadukayo
katika kuongea kwao na kupinga ufufuko, wanachukua maisha ya mtu duniani na
kuyafanya kuwa ni maisha ya mbinguni, walidhani kwamba kama kuna maisha baada
ya kifo, basi kuoa na kuolewa kutaendelea huko pia. Jibu la Yesu lina sehemu
mbili, “hawaoi wala hawaolewi kwasababu hawatakufa tena”-Yesu anataka kuwaambia
kwamba kuoa na kuolewa inatakiwa hapa duaniani kwasababu wanadamu na uwepo wetu
hapa ni wa muda tu. Kwahiyo, ndoa ni jambo jema ambalo mwanadamu anategemeza.
Lakini katika maisha yajayo, hatufi tena kwahiyo Yesu anasema kwamba hakuna
ndoa baada ya maisha haya. “Kwani watakuwa sawa na malaika”-baada ya kufa
hatubebi tena miili yetu ambayo imeumbwa kuikabili dunia na tamaa zake bali
tunakuwa na miili ya ufufuko, miili ya utukufu (kama ile ya malaika) na hivyo
kuwa huru kuhusu mambo yote ya duniani au yote tulionayo hapa duniani . Kwahiyo
hakuna ndoa katika maisha yajayo.
Katika sehemu ya pili, Yesu anatoa kithibitisho
kutoka katika kitabu cha Kutoka, tunakopata habari ya Musa kukutana na Mungu
katika kichaka kinacho waka moto. Yesu itakuwa aliamua kuchagua kutoa jibu lake
kutoka katika kitabu hiki kusudi kabisa kwasababu Masadukayo wali amini tu
Tora. Masadukayo waliamini kuhusu Mababu, kama Abrahamu, Isaka, Yakobo- ambao
majina yao Musa aliyatamka katika mlima Sinai. Yesu anasema kuwa “kwakuwa Mungu
sio wa waliokufa bali wanaoishi”, Abrahamu, Isaka na Yakobo lazima watakuwa
wanaishi hata baada ya kufa kwao. Kwakutengeneza majibu ya namna hii kutoka
katika maandiko, Yesu aliwanyamazisha Masadukayo, kama ilivyo andikwa katika
kitabu cha Methali 26:27 –“kila achimbae shimo atatumbukia humo mwenyewe”.
Masadukayo walichimba shimo ili kumtega Yesu lakini wao wenyewe wametumbukia
humo.
Tuna ujumbe unaoendana katika somo la kwanza
kutoka katika kitabu cha pili cha Makabayo tunaposikia kuhusu kifodini cha
ndugu saba Wayahudi, ambao walikataa kuikana dini yao. Hawa 7 walitoa maisha
yao wenyewe huku wakitangaza Imani yao juu ya ufufuko- mmoja wao alilia kwa
sauti akisema “tutafufuliwa naye”. Mara nyingi tunaongea kuhusu maisha ya
duniani kuwa mazuri kuishi lakini hapa tunaona Imani ya pekee kutoka kwa hawa
ndugu saba wanao tufundisha kuhusu maisha ya umilele ambayo tutarithi
tunastahili kufa kwa ajili ya hayo. Habari hii ya ndugu saba inatupa matumaini
kwamba sisi nasi twaweza kuitangaza kama wao “tunakufa, ili tukaishi tena milele”
. Ni hakika kwamba, kwa akili zetu zilizo na mipaka maisha baada ya kifo ni
fumbo kubwa lisilo na jibu. Tunakuwa na mashaka na kuacha kuongea tunapo fikiri
kuhusu ufufuko na maisha baada ya kifo, kwakuwa sisi ni wanadamu kama
ilivyokuwa kwa wanafunzi baada ya kifo cha Yesu. Lakini walicho shikilia ni
“tumaini’ na ni kitu ambacho sisi wote tunapaswa kushikilia. Kwahiyo tukiwa
tumejazwa na Imani na matumaini tuamini alichotuambia Yesu –“ninaenda
kuwaandalia makao”, kwasababu kila alichosema Yesu ni kweli tupu na alimanisha.
Tunapo elekea mwishoni mwa mwaka wa huruma ya
Mungu tunapaswa kusisitiza ujumbe huu wa maisha baada ya maisha ya hapa
duniani. Lakini kivipi? Tunatambua kuhusu matendo ya huruma aliotusisitizia
Papa Fransisko kufanya, baadhi ya hayo ni kuwalisha wenye njaa, kuwavisha wasio
na nguo, kuwatembelea wagonjwa na wafungwa, kuwasaidia maskini nk. Imani yetu
kuhusu maisha yajayo inaimarishwa ndani mwetu na fadhila ya matumaini na
kwakufanya matendo ya huruma kwasababu tunaenda kuwapa tumaini hili hili
wengine waliolipoteza.
Sala: Bwana Yesu, naomba
niwe mjumbe wa matumani kwa ndugu zangu, na hasa kwa wale wanaoteseka. Amina.
No comments:
Post a Comment