Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

THAMANI YA WAKATI WA SASA!




























“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Oktoba, 22, 2022
Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Yohane Paulo II, Papa

Ef 4:7-16;
Zab 121:1-5;
Lk 13:1-9


THAMANI YA WAKATI WA SASA!

Majanga au ajali katika maisha ya watu mara nyingi zinawafanya wajiulize maswali kama vile, kwanini? Au kwanini wao? Katika Injili ya leo Yesu anaeleza juu ya tukio baya lililosababisha vifo vya baadhi ya Wagalilaya waliouwawa na jeshi la Warumi chini ya utawala wa Kamanda Pilato. Kipindi flani watu walisema kwamba hii ilikuwa adhabu ya Mungu kwa hawa watu kwasababu ya maadili yao mabaya. Yesu anakataa akisema mwadhani walikuwa ni wakosefu kuliko watu walioishi Yerusalemu? “Kwahakika hapana!” Alisema. Kwa uhakika anawaambia Wafuasi wake kwamba nao watakutana na mambo kama hayo wasipobadili mienendo yao. Dhambi za waliokufa haikuwa sababu ya kifo chao, bali ni onyo kwetu ili kuona kama tupo tayari kwa tukio kama hilo.

Yesu anaendelea akielezea maana ya hayo akitumia mfano wa Mtini. Katika taswira watu aliokuwa anaongea nao walikuwa kama mtini ambao haujazaa matunda. Miaka mitatu iliyotajwa katika mfano huu inaweza kulinganishwa na urefu wa miaka mitatu ya utume wa Yesu. Lakini, bado wana muda wakuchunguza maisha yao, muda ambao hawakupewa wale waliokufa katika matukio yale mawili. Sisi nasi tumepewa muda- siku? Mwezi? Miaka mingi? Hatuna habari juu ya hilo. Lililo wazi ni kwamba hamna muda wa kupoteza, tunaanza leo, na zaidi sana sasa hivi. Kwa Mungu, miaka iliyopita haijalishi wala si maisha ya baadaye, kinacho jalisha ni “sasa”. Kama nipo naye sasa katika maisha yangu, sina chochote cha kuhofia.

SALA: Bwana nisaidie niweze kutumia vizuri muda ulionipa, niweze kubadili maisha yangu. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment