MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 23, 2022
DOMINIKA YA 30 YA MWAKA C WA KANISA
Wimbo wa Mwanzo: Zab. 105:3-4
Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. Mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
SOMO 1
YbS. 35:12 – 14, 16 – 19
Kwa kuwa Bwana ndiye mhukumu wala hakijali cheo cha mtu. Hatamkubali yeyote juu ya maskini, naye ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa. Hatayadharau kamwe Malalamiko ya yatima, wala ya mjane amwelezapo habari zake. Malalamiko yake aliyeonewa yatapata kukubaliwa, na dua yake itafika hima mbinguni. Salsa yake mnyenyekevu hupenya mawingu; wal ahaitatulia hata itakapowasili; wala haitaondoka hata Aliye juu atakapoiangalia, akaamua kwa adili, akatekeleza hukumu. Wala Bwana hatalegea, wala hatakuwa mvumilivu kwa wanadamu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34: 1 – 2, 16 – 18, 22 (K) 6
(K) Maskini huyu aliita Bwana akasikia.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi. (K)
Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Ili aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwana akasikia.
Akawaponya na taabu zao zote. (K)
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. (K)
SOMO 2
2Tim. 4:6 – 8, 16 – 18
Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda: baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote, pia waliopenda kufunuliwa kwake. Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
SHANGILIO
Yn. 8:12
Aleluya, aleluya!
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
INJILI
Lk. 18:9 – 14
Yesu aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma;p hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
No comments:
Post a Comment