Jumamosi, Septemba 17, 2022
Juma la 24 la Mwaka
1 Kor 15: 35-37, 42-49
Zab 55: 10-14
Lk 8: 4-15
UFUFUKO: LENGO LA MAISHA YETU!
Katika somo la kwanza Mt. Paulo anaelezea kuhusu tatizo la kutoamini ukweli wa ufufuko. Mtakatifu Paulo anaeleza wazi wazi kwamba ufufuko wa wafu ni ukweli halisi ambao imani yetu imejikita. “Kama hamna ufufuko wa wafu” anasema, “Yesu hakufufuka… na Imani yenu ni bure” (1 Kor 15: 13-14). Tunafufuliwa na mwili wa utukufu, ambao ni tofauti na mwili tunao uona. Mwili tunao uona unaisha na ni dhaifu, mwili wa utukufu hauharibiki kamwe, wenye nguvu na uliofufuliwa kwa utukufu. Hili ndilo tunalo amini kama Wakristo, tunalolitazamia kuwa na kuishi kwalo.
Mungu amemuumba kila mtu ili aweze kuingia katika utukufu wa ufufuko ‘ili awe naye milele katika maisha ya umilele Mbinguni’. Lakini pia Injili inaelezea mfano wa jinsi wengi wetu kama mbegu tunashindwa kulipata lengo hili. Ufufuko ni zawadi, sio haki, na utapewa kwa wale walio kama mbegu zilizo anguka kwenye udongo mzuri, wanaozishika kweli amri za Bwana, “kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.” Ni juu yetu kukubali au kukataa wema huu mkuu wa Mungu kwetu. Tutumie uhuru wetu vizuri tuweze kuchangua kuwa mbegu zuri na tulio ota katika udogo wenye rutuba. Maisha yetu yawe yanamtumainia Yesu kila siku, lakini tunapaswa kumwagilia kwa sala, kusoma neno lake, kuishi vyema na ndugu zetu, uvumilivu katika changamoto za maisha, kwa njia hiyo tutasitawa na kumea na kuzaa matunda mema daima. Na mwishowe tutazaliwa upya katika ufalme wa Mungu (ufufuko) baada ya maisha yetu hapa duniani.
Sala: Bwana, nashukuru kwa zawadi ya ufufuko. Naomba unifanye nistahili kuupokea. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment