“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Septemba 30, 2022
Juma la 26 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Jeromu, Padre na Mwalimu wa Kanisa
Ayu 38: 1, 12-21, 40:3-5
Zab 139: 1-3, 7-10, 13-14
Lk 10: 13-16
NENO LA MUNGU
Imekuwa kama fasheni siku hizi mtu kuulizia kuhusu uwepo wa Mungu. Huku wakirejea mateso na maovu yaliopo ulimwengu, kiasi cha kuwafanya watu wengine kuwa vigumu kumtafuta au kuwa karibu na Mungu. Kadiri ya watu wanao jiita wa kisasa, mtu amejifanya mwenyewe kwasababu akili imeshindwa kuoanisha kati ya Mungu anayetupenda na maovu yanayotendeka katika jamii, wanaona ni vizuri kuachilia mbali swala la Mungu au kumkataa. Kitabu cha Ayubu kinajibu baadhi ya maswali juu ya uwepo wa Mungu mwema anayetupenda na uwepo wa maovu ulimwenguni. Ayubu mtu mwaminifu na aliyejikita kwa Mungu anateseka vikali katika mikono ya yule muovu. Marafiki zake wanahitimisha kwamba ni kwasababu ya dhambi zake. Lakini , Ayubu alitambua kwamba alikuwa sahihi, na ndio maana alijaribu kumuuliza Mungu yeye mwenyewe! Katika somo la leo Mungu anamjibu Ayubu! Ingawaje majibu ya Mungu yamejitengeneza katika hali ya maswali, bado Ayubu anafurahia majibu hayo. Ayubu alitaka kuwa na uhakika juu ya sababu ya mateso yake. Kama ni Mungu amependa ateseke, yeye alikuwa tayari.
Leo tuna adhimisha kumbukumbu ya Mt. Jeromu, ambaye anajulikana kama Baba wa Sayansi ya Biblia. Hii ni kwasababu alikuwa ni yeye aliye tafsiri Biblia ya Kiebrania, Agano la Kale na Kigiriki, Agano Jipya kwenda kwenye “Vulgate” tafsiri ya Kilatini. Alisema kwa hakika: “kutokufahamu maandiko ni kutokumfahamu Kristo”. Katika Kanisa tuna heshimu Maandiko Matakatifu katika hali ya juu, lakini Imani yetu sio “Imani ya Kitabu” tu, bali mapokeo ya mababa wa Kanisa na mafundisho yake (Sacred Traditions). Pia maneno ya Mungu sio maneno yalioandikwa na kuachwa kitabuni bali ni maneno yalio hai, yanayogusa maisha ya watu ambayo yana mwilishwa na watu na kuyaishi. Mungu anaongea nasi kama anavyo ongea na Ayubu kwa kupitia Kristo. Je, Kristo ni ‘Neno anayeishi’ kwako na kwangu?
Bwana: Bwana, niongoze kwenye Neno lako kwa njia ya Neno wako. Amina

Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment