Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUTUMIKIA MUNGU NA JIRANI!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Septemba 22, 2022 
Juma la 25 la Mwaka


Mhu 1: 2-11
Zab 89: 3-6, 12-14, 17
Lk 9: 7-9


KUTUMIKIA MUNGU NA JIRANI!

Katika somo la Injili ya leo, tunasikia Herode, akifadhaika baada ya kupata habari kuhusu Yesu. Alama iliyo baki katika dhamiri yake bado inaendelea kumkumbusha kuhusu damu aliyo mwaga ya mtu asiye na hatia ya Yohane Mbatizaji. Sehemu ya pili ya Injili pia inatueleza nini kinacho leta furaha –kumtumikia Bwana, na pia kuwafikia wengine. 

Maisha ya Herodi hayakukosa chochote cha anasa na maisha ya kujiburudisha. Lakini, watu hawakuwa wanaongea kuhusu yeye. Wote walikuwa wakiongelea kuhusu Kristo. Baba Mtakatifu mstaafu Benedict wa XVI alisema “Kanisa linalo tafuta kuwa kivutio na maarufu kuliko yote tayari lipo katika njia isio sahihi, kwasababu Kanisa halifanyi kazi kwa ajili yake binafsi, halifanyi kazi ili kuongeza idadi ya watu na nguvu zake. Kanisa lipo kwa ajili ya kuwatumikia watu. Halijitumikii, halitumikii ili kuwa lenye nguvu, bali, linatumikia ili kumtangaza Yesu Kristo: ukweli mkuu, nguvu kuu ya upendo na msahama unao jionesha kwake na ambao unatokea kila wakati kwa uwepo wa Yesu Kristo” 

Sala: Bwana, niongezee tamaa yangu ya kufanya mapenzi yako na kuwatumikia wengine kwa mapendo. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment