MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, 24 Julai, 2022
Dominika ya 17 ya Mwaka C wa Kanisa
Mw 18: 20-32;
Zab138: 1-3, 6-8;
Kol 2: 12-14;
Lk 11: 1-13.
BABA YETU!
Wayahudi walijulikana kwa majitoleo yao kwenye sala. Sala ilielezewa katika
nyakati tatu. Marabi walikuwa na sala ya kila tukio. Ilikuwa pia ni utamaduni
wa Marabi kuwafundisha watu sala mbali mbali ili waweze kuzitumia katika hali
zao na nyakati mbali mbali katika maisha ya kila siku. Wafuasi wa Yesu
walimuuliza pia Yesu kuhusu sala. Wakati Yesu alipowapa sala aliwapa sala ya
mfuasi tunayoiita Baba yetu au Sala ya Bwana. Kila kipengele kinaweza kusimama
chenyewe nakujitosheleza kama kifungu cha sala. Tuangalie utajiri wa sala hii:
Baba
Inaanza kwakumuonesha Mungu kuwa ni "Baba". Hatumuiti Bwana au
mkuu au Hakimu. Wala hatumuiti, chanzo cha hekima yote, au Muumbaji Bali
tunamuita kwa jina la nafsi, Baba, tusipo lipokea hili kama ukweli halisi,
itakuwa vigumu kwetu kumuita Mungu " Baba yetu na sio Baba yangu. Kama
tutakavyoona Sala ya Bwana ni zaidi ya
sala ya kuomba. Ni sala inayo onesha sisi ninani na sisi nini kwa Mungu na kwa wenzetu.
Jina lako litukuzwe
Kwa Wayahudi jina haikuwa tu
kiashiria cha kitambulisho. Wakati Musa akiongea na Mungu katika kichaga
kilicho waka moto, alitaka kujua jina la Mungu ili afahamu ni nani. Kwanjia
nyingine pia ninani anaweza kumfanya Mungu Mtakatifu au jina lake Takatifu?
Utakatifu wake hautegemeani na sisi kwa njia yeyeyote. Tunachoomba sisi ni
kwamba sisi tukiri utakatifu wake sio tu kwa maneno pia kwa njia ya maisha
yetu.
Ufalme wako ufike
Ufalme wa Mungu tunaweza kuuelewa kama ulimwengu ambamo kila kitu
anachosimamia Mungu kinakuwa na uhalisia kamili katika maisha ya watu kila
mahali–ulimwemgu uliojengwa katika ukweli, upendo, huruma, haki, uhuru, utu wa
kibinadamu, na amani. Ufalme upo mbali tunashindwa kuona uhalisia huu, na
wakulaumiwa ni sisi wenyewe. Kwahiyo tunaposema maneno haya hatuombi tuu msaada
wa Mungu bali tunajikumbusha wenyewe katika kushiriki kufanya kazi na Mungu
ili kufanya Ufalme huo uwe uhalisia wa
kweli.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Nusu ya pili ya sala tunasali zaidi kwaajili ya mahitaji yetu. Tambua
tunaomba kwaajili ya mkate, chakula, chetu cha siku, mahitaji yetu ya kila
siku. Je, tunaomba kwaajili hiyo? Au
hofu zetu zinatufanya tuombe mpaka cha siku nyingi zijazo? Hata hivyo kwakusali
namna hii inaelezea imani yetu juu ya Mungu kutujali sisi. Hakuna sababu ya
mashaka na wasiwasi kuhusu wakati ujao katika kumtumainia Mungu.
Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyo wasamehe waliotukosea
Hapa tunasali kwakuomba toba ya makosa yetu tuliyotenda ila sala yetu
ina masharti, ikituunganisha tena na
wale walio karibu yetu. Tunaomba Mungu atusamehe kwa Yale tulioenda kinyume na
kukosea, kwasababu tumesha wasamahe wale wote ambao tunajisikia wametukosea.
Tunaomba kushiriki katika hali nzuri ya sifa ya Mungu– utayari wake wa kusamehe
sio tu "saba mara sabini" bali kusamehe bila kikomo.
Usitutie katika Kishawishi
Na hatimaye tunaomba tukingwe na vishawishi vijavyo ambavyo vinaweza
kutukumba sisi. Vishawishi hivi na majaribu
haya yanaweza kutufanya tuanguke na tushindwe kumfuata yeye.
Pengine tunaweza kukubali kwamba hatuitendei haki sala hii wakati mwingine.
Sala hii haituweki tu karibu na Mungu bali inatuweka wamoja na karibu sisi kwa
sisi. Tukiwa tunaendelea kusali sala ya Bwana, ingekuwa vizuri na manufaa kama
tutaisali taratibu, ombi moja baada ya jingine, na hata kutafakari ili iwe na manufaa kwetu na Mungu
atukuzwe.
Sala: Baba yetu uliye Mbinguni jina lako litukuzwe. Amina.
No comments:
Post a Comment