“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Ijumaa, Aprili 21, 2023
Juma la 2 la Pasaka
Mdo 5:34-42
Zab 27: 1,4,13-14
Yn 6:1-15
KUFAULU KATIKA JARIBIO LA IMANI!
Mungu daima anatambua anachopenda kufanya. Daima yeye ana mpango mkamilifu
wa maisha yetu. Leo katika Injili, Yesu anafanya muujiza wa kuwalisha watu kwa
mkate na samaki. Yesu alitambua kwamba ataongeza mkate na samaki ili kuwalisha
watu zaidi ya elfu tano. Lakini kabla ya kufanya hili, anamjaribu Philipo.
Hivyo hivyo Yesu anatujaribu wakati mwingine. Je, hafanyi hivyo?
Majaribio haya sio kwamba Yesu anapenda kutuuliza tu au kufanya mchezo
Fulani na sisi. Bali, anatupa nafasi ya kudhihirisha imani yetu kwake. Jaribio
lililopo kwenye Injili lilikuwa ni kumfanya Philipo atumie Imani zaidi kuliko
kufikiri kwa kawaida pekee. Philipo aliitwa ili kudhihirisha imani kwamba Mwana
wa Mungu yupo pamoja nao pale. Lakini alishindwa jaribio. Alinyoosha mkono kwa
ile hali ya kutokuwezekana. Lakini katika hali nyingine ni kama Andrea alikuja
kuokoa. Anasema kuna kijana hapa ana mkate na visamaki vichache. Lakini yeye
pia alikuwa na Imani kidogo, aliongeza kusema “lakini vya faa nini kwa umati
huu mkubwa namna hii?”.
Chembe hii dogo ya imani ya Andrea, ilitosha kwa Yesu kuamuru watu waketi
makundi makundi na hivyo kufanya ule muujiza. Inaonekana kwamba Andrea alikuwa
na ufahamu kidogo kwamba ilikuwa muhimu kutaja visamaki hivi na mkate. Yesu
anavichukua kutoka katika mikono ya Andrea na kuwajali watu.
Mara nyingi tunajikuta katika hali ngumu na hatujui tufanye nini. Tunapaswa
kujitahidi kuwa na imani kidogo ili Yesu aweze kuwa na kitu cha kutenda katika
maisha yetu. Tunaweza tusiwe na ufahamu wa nini anaenda kufanya, lakini ni
lazima kuwa na ufahamu hata kidogo kwamba Mungu ndiye anaye tuongoza sisi. Kama
tutaweza hata kukuza Imani hii kidogo sisi pia tutashinda majaribio.
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuwa na Imani kamili ya mpango wako ambao
unapenda kuufanya katika maisha yangu. Nisaidie niweze kufahamu kwamba wewe
unaongoza na kuyalinda maisha yangu hata pale ninapo ona maisha yanayumba.
Katika hali hizo, ninaomba Imani ninayo onesha iwe zawadi kwako ili uweze
kuitumia kwa utukufu wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment