MASOMO YA MISA,
JUMANNE, AGOSTI 17, 2021
JUMA LA 20 LA MWAKA
________
SOMO I
Amu 6: 11-24
Malaika wa Bwana alienda
akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi,
Mwabiezeri;na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili
kuficha machoni pa Wamidiani. Malaika wa bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu
pamoja nawe,Ee shujaa. Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu,ikiwa bwana yu pamoja
nasi na mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu,
waliotuhafithia babu zetu,wakisema, Je! Siye bwana aliyetuleta huku kutoka
Misri? Ila sasa ametutupa,naye ametutia katika mikono ya Midiani. Bwana
akamtazama, akasema,enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa
Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa
jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi
ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. Bwana akamwambia, hakika
nitakuwa nawe, nawe utawapiga Wamiadini
kama mtu mmoja. Naye akamwambia, kama nimepata kibali mbele za macho
yako, basi unionyeshe ishara, ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami. Tafadhali
usiondoke hapa hata nikujue, nikatoe
zawadi yangu, na kuiweka mbele zako.
Akasema, Nitangoja hata
utakaporudi. Basi Gideoni akainhia ndani,akaanda mwna-mbuzi, na mikate
isiyotiwa chachu, ya efa ya unga;akaitia ile nyama katika kikapu,akautia mchuzi
katika Nyungu, akamletea hapo nje chini ya mwaloni, akampa. Naye Malaika wa
Mungu akamwambia, itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu uiweke juu ya mwamba
huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo. Ndipo malaika wa bwana akanyosha
ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na mikate;malaika
wa bwana akaondoka mbele ya macho yake. Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa
bwana. Gideoni akasema,Ole wangu, Ee Bwana Mungu!kwa kuwa nimemwona Bwana uso
kwa uso . Bwana, akamwambia,Amani iwe pamoja nawe;usiogope hutakufa. Ndipo
Gideoni akamjengea bwana madhabahu hapo, akaita jina lake, Yehova shalomu; hata
hivi leo iko huko Ofra ya Waabiezeri.
Neno la
Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 85: 8, 10-13
(K) Bwana atawambia watu
wake amani.
Fadhili zake na uaminifu
vitakutana;
uadilifu na amani
vitaungana.
Uaminifu utachipuka
katika nchi;
uadilifu utashuka toka
mbinguni. (K)
Mwenyezi-Mungu atatuletea
fanaka,
na nchi yetu itatoa mazao
yake mengi.
Uadilifu utamtangulia
Mungu
na kumtayarishia njia
yake. (K)
________
SHANGILIO
1 Thes. 2:13
Aleluya, aleluya,
Lipokeeni neno la Mungu,
siyo kama neno la
wanadamu,
bali kama neno la Mungu.
Aleluya
________
INJILI
Mt. 19: 23-30
Yesu aliwambia Wanafunzi
wake, Amini,nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme
wa mbinguni. Nawambia tena, ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupenya tundu la
sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanafunzi wasiposikia,
walishangaa mno, wakisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho,
akawambia, kwa mwanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata;
tutapata nini basi? Yesu akawambia, Amini, nawaambia ya kwamba ninyi
mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti
cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu
kabila kumi na mbili za Israeli. Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa
kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto au mashamba, kwa ajili ya jina
langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele. Lakini wengi walio wa
kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment